Bilinganya na paja Nguruwe lililokaushwa
MAHITAJI
a/ Paja la nguruwe lililokaushwa
b/ Bilinganya moja
c/ Pilipili mboga moja
d/ Pilipili hoho moja
e/ Tangawizi gramu 5
f/ Chumvi gramu 10g
h/ Sukari gramu 2
i/ Mchuzi wa soya kijiko kimoja na maji ya wanga
JINSI YA KUTENGENEZA
Kata paja la nguruwe lililokaushwa na liwe vipande kisha kata bilinganya iwe vipande virefu, kata pilipili mboga na pilipili hoho ziwe vipande pia.
Baada ya hapo washa moto weka mafuta kwenye sufuria mpaka yawe na joto la nyuzi ya sentigred 60, tia vipande vya tangawizi, pilipili mboga, pilipili hoho, korogakoroga, tia vipande vya paja la nguruwe lililokaushwa.
Kisha endelea kukoroga koroga, tia vipande vya bilinganya, huku ikikoroga weka chumvi, sukari, mimina mchuzi wa soya halafu mimina maji ya wanga korogakoroga na kabla ya kupakua mimina mafuta ya ufuta. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
Imeandaliwa na Jacqueline

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala