Mapishi ya samaki na bilinganya
MAHITAJ I
a/ Samaki mmoja
b/ bilinganya 1
c/ chumvi vijiko viwili
d/ chembechembe za kukoleza ladha kijiko 1
e/ mchuzi wa sosi vijiko 2
f/ pilipili manga kijiko 1g/ vipande vya vitunguu maji
h//pilipili hoho, tangawizi , sosi ya pilipili hoho vijiko 1.
JINSI YA KUTENGENEZA
1.Ondoa vitu vilivyo ndani ya tumbo la samaki, halafu osha samaki na kumkata awe vipande baada ya hapo kata bilinganya liwe vipande na
washa moto weka sufuria motoni, tia vipande vya bilinganya vikaange halafu vipakue.
2.Weka vipande vya tangawizi na sosi ya pilipili hoho korogakoroga, halafu tia vipande vya samaki huku ukiendelea kukoroga huku ukimimina maji baada ya kuchemka, tia chumvi kiasi.
3.Weka pia chembechembe za kukoleza ladha na uendelee kukorogakoroga, tia vipande vya bilingaya, na pilipili hoho korogakoroga halafu punguza moto kidogo, baada ya dakika 15, tia mchuzi wa sosi na maji ya wanga korogakoroga mpaka ichemke baada ya muda ipakue.
4.Na mwisho weka vipande vya vitunguu maji na pilipili hoho na baada ya hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.