Suti ni Vazi la jinsia zote
Vazi la suti ni vazi linalompa hadhi mvaaji na huvaliwa kwenye hafla mbalimbali katika wakati maalumu hasa kwenye hali ya hewa ya baridi.
Vazi hili ambalo mbali a kumpa hadhi mvaaji na kuvaliwa katika sehemu maalumu, pia lina masharti yake, ambapo mvaaji anatakiwa kuzingatia vazi ili asilishushe hadhi pindi anapokuwa amevaa.
Baadhi ya watu hufikiria vazi hili huvaliwa na watu maalumu kama viongozi mbalimbali wa serikalini, wafanyakazi wa mahakama na wengineo, la hasha!! pia huvaliwa na watu tofauti na hao. Kwani vazi hili mara nyingi sehemu za ofisini basi utalifurahia vazi hili kama utalivaa katika ofisi yenye kiyoyozi kwa kuwa lina leta joto.
Kama ofisi yako ikiwa na kiyoyozi ni vyema endapo utavaa suti kwa kuwa hewa inayotokana na kiyoyozi hicho inaweza kuwasababishia madhara hapo baadaye.
Suti ni vazi maalumu ambalo pia huvaliwa na maharusi pndi wanapokuwa kwenye sherehe za kufunga ndoa, na humpendezesha bwana harusi kwani humfanya kuonekana tofauti.
Endapo kama utavaa vazi hili katika hali ya joto utalichukia na kutamani kulivua, kwani utatamani kulivua kutokana na joto lake.
Suti inapendeza sana kuvaliwa na viatu virefu kwa wanawake ambavyo vimezibwa mbele na kwa wanaume wanatakiwa kuvaa suti huku wakiwa wamevaa viatu vilivyozibwa sambamba na soksi na hapo utaonekana maridadi sana.
 |

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala