Tafuta DHWTangazaTuandikie
Mapishi ya mseto wa kuku

MAHITAJI

a/ Pilipili mboga 1
b/ Kuku mmoja
c/ Yai moja
d/ mboga gramu 20
e/ vitunguu maji gramu 5
f/ Mchele kilo 1
g/ Sosi ya kambamti gramu 5
h/ Chumvi
i/ Tangawizi pamoja na kitunguu sahumu
j/ Nyanya kiasi

JINSI YA KUTENGENEZA PISHI LAKO

1. Kwanza kabisa kata pilipili mboga na nyama ya kuku iwe vipande vipande na kisha livunje yai na ulikoroge hilo yai,andaa tangawizi pamoja na kitunguu sahumu kwa kuvitwanga.

2. Baada ya hapo unaweza kuwasha moto wako kuichemsha nyama yako ya kuku ukiweka tangawizi, kitunguu sahumu pamoja na chumvi ili iweze kulainika vizuri, baada ya muda itakuwa teyari kwani waweza kuepua nyama yako baada ya hapo injika sufuria yako jikoni, weka mafuta kiasi na kisha mimina yai lililokorogwa ulikaangae na uweze kulipakua kwenye sahani.

3. Bandika tena sufuria jikoni na uweke mafuta kiasi kwa ajili ya kukaanga vipande vya vitunguu maji huku ukiendelea kukoroga weka nyanya ulizo ziandaa mpaka ziive kisha weka vipande vya nyama ya kuku huku ukikoroga.

4. Baada ya muda mboga na vipande vya pilipili mboga, sosi ya kambamti, huku ukiendelea kukoroga weka wali na kisha punguza moto na ukoroge kwa haraka huku ukiweka chumvi kiasi na chembechembe za kukoleza ladha huku ukikorogo na baada ya muda chakula chako kitakuwa teyeri kuipuliwa na hata kupakuliwa na kuanza kuliwa pia.




Imeandaliwa na Jacqueline


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.