Tafuta DHWTangazaTuandikie
Pishi la nyama ya ng'ombe kwa mvuke

MAHITAJI

a/ Nyama ya ng'ombe kila 1 1/2
b/ Mafuta ya kula saizi itoshayo kupikia
c/ Mchuzi wa sosi gramu 30
d/ Unga wa pilipili hoho gramu 3
e/ Unga wa mchele 75
f/ Unga wa pilipili manga gramu 2
g/ Vitunguu maji na tangawizi kila kimoja gramu 8


JIMSI YAKUPIKA PISHI LENYEWE

1. kata nyama ya ng'ombe iwe vipande vyembamba, kata vitunguu maji, saga tangawizi halafu weka kwenye maji kidogo sana ili utakapo ikamulia kwenye nyama iweze kutoa maji mazito, koroga vipande vya nyama ya ng'ombe pamoja na mafuta.

2. Weka mchuzi wa sosi, tangawizi, unga wa pilipili manga, unga wa mchele, halafu weka kwenye bakuli.

3.Kisha mimina maji kiasi kwenye sufuria na uweke bakuli hiyo kwenye sufuria, washa moto na uchemsha kwa mvuke na baada ya kuiva pakua na uweke nyama ya ng'ombe kwenye sahani na kisha weka vipande vya vitunguu maji, unga wa pilipili hoho.

Wadau wangu mpaka hapo kitoweo hiki kitakuwa kiko tayari kwa kupakuliwa na kuanza kuliwa.




Imeandaliwa na Jacqueline Moshi



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.