Pishi la samaki kwa unga wenye ladha ya viungo vitano
MAHITAJI
a/ Samaki mmoja
b/ kiasi kidogo cha vitunguu maji na tangawizi
c/ Mvinyo wa kupikia kijiko kimoja
d/ Mchuzi wa soya vijiko viwili
e/ Unga wenye ladha ya viungo vitano
f/ Sukari kijiko kimoja
g/Mafuta ya ufuta kijiko kimoja na chumvi kijiiko moja.
UANDAAJI NA UPIKAJI WA PISHI LENYEWE
1. Kwanza kabisa ondoa uchafu uliopo ndani vya samaki baada ya hapo mwoshe halafu mkate awe vipande, iweke pamoja na mchuzi wa soya, chumvi, mvinyo wa kupikia, vitunguu maji na tangawizi.
2. Baada ya hapo washa moto, kisha weka mafuta kwenye kikaangio cha samaki mpaka yawe joto la nyuzi 70, kaanga vipande vya samaki mpaka viive na kisha vitoe.
3. Baada ya hapo epua kikaangio chako cha samaki na kisha bandika sufuria nyingine ambayo ni safi na kisha uweke mafuta kiasi kwa ajili ya kuweka vipande vya vitunguu maji, tangawizi korogakoroga, mimina mvinyo wa kupikia, mchuzi wa soya, maji, chumvi, M.S.G, sukari, unga wenye ladha ya viungo vitano, siki na vipande vya samaki, baada ya kuchemka, punguza moto na endelea kuchemsha kwa dakika 30, halafu vipakue.
4. Weka vipande vya samaki kwenye sufuria, chemsha kwa mvuke kwa dakika 15, vipakue na mimina mafuta ya ufuta.
Na mpaka hapo pishi lako litakuwa teyari kwa kuepuliwa na hata kuliwa pia.
Imeandaliwa na Jacqueline Moshi

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala