Tafuta DHWTangazaTuandikie
Je wafahamu kitambaa cha Satin hushonea nguo za aina gani?

Kitambaa aina ya Satin siyo kigeni kwa miaka mingi, kwani kimekuwa kikitumika katika kushonea mavazi iwe kwa mwanamke au hata kwa mwanaume. Kitambaa hiki cha Satin pia hutumika katika kupambia kwenye Maharusi hata kwa kutandikia kitandani kama shuka, kwani hata watoto pia huvaa mavazi yatokanayo na matirio ya Satin.

Kama nilivyofafanua hapo juu kwamba kitambaa hiki kimekuwa kikitumika katika kushonea nguo hasa za usiku na hata pia magauni ya maharusi kwasababu ya mng'ao wa kitambaa hicho.

Pia kitambaa hiki hutumika hasa kwa kushonea nguo za kulalia, nguo za ndani, bukta za wanariadha, jezi za mpiwa wa kikapu na kadhalika, lakini kutokana na mapinduzi katika ulimwengu wa mitindo kitambaa hiki hivi sasa kimeanza kutumika kushona nguo mbalimbali za mchana hasa blauzi z wanawake.

Pia kuna mashati yaliyoshonwa kwa kitambaa cha Satin yawe ya mikono mifupi au hata mirefu, kwani yapo kwenye chati na mvaaji huonekana mtanashati.

Kuna mavazi mengine ya Satin kama vile Suruali, Sketi na hata Magauni kwani hayapo kwenye chati ingawa siyo vibaya yakivaliwa iwapo yakimpendeza muhusika. Kama unataka kwenda na wakati basi nakushauri uvae shati la Satin na suruali ya kitambaa inayofika tumboni, na ikibidi chomekea shati lako kwani utatoka bomba sana.

Usipitwe na wakati wa vaa shati la satin hasa kwa kuwa ni moja kati ya mavazi ambayo huuzwa kwa bei rahisi, kwani humfanya mvaaji aonekane mtanashat zaidi na anyekwenda na wakati.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.