KISHUMBA
MAHITAJI
a/ Ndizi za mshare kichane kimoja
b/ Vikombe viwili vya maharage
c/ Magadi
c/ Chumvi
d/ Robo kikombe cha mafuta ya kupikia
UANDAAJI PAMOJA NA UPIKAJI WAKE
1.Chagua maharage yako na kisha uyaoshe vizuri kisha uyainjike jikoni na uhakikishe yasiive sana.
2.Baada ya kuinjika maharage hayo, anza kumenya ndizi na kisha uzikatekate vipande vidogodogo na uzioshe kwa uangalifu baada ya hapo changanya ndizi hizo pamoja na maharage ambayo yanatakiwa yasiive sana.
3.Baada ya hapo katakata nyanya, vitunguu, karoti, chumvi, mafuta pamoja na binzali kisha weka maji kiasi ufunike na kukiinjika jikoni.
4.Baada ya muda unatakiwa kuongeza maji kidogo ili kuhakikisha ndizi zinaiva taratibu, baada ya kucheki tena na kukuta kuwa zinakaribia kuiva basi weka tui la nazi huku ukiendelea kukoroga ili tui lisikatika, na baada ya muda moto na ukiachejikoni kiendelee kuiva taratibu kwa dakika kumi.
Baada ya hapo msosi wako utakuwa umeshaiva kwani ruksa kuipua chakula chako kukipakua na kuanza kula wewe pamoja na familia yako.
Imeandaliwa na Jacqueline

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala