Mbunifu Mchanga mwenye nyota nzuri
Ally Rehmtullah ni kijana mchanga mwenye umri wa miaka 23, kwani nyota yake imeanza kung'ara katika masuala mazima ya ubunifu katika mitindo mbalimbali kwa hapa nchini Tanzania.
Ameanza kuvuma katika masuala ya ubunifu wa mavazi kwani ni kijana mdogo sana kati ya vijana wa Kitanzania, ameamua kufanya kazi tofauti sana na vijana wa chimbuko la sasa wanavyofanya.
Kwa kweli ni mara chahe sana ukamkuta kijana wa Kibongo 'kitanzania' mwenye umri wa miaka kama 19 na kuendelea, akijishughulisha na shuhuli nyingine tofauti na muziki au sanaa ya maigizo.
Katika masiha ya sasa vijana wengi wameamua hata kuacha masomo yao na kujipachika katika masuala ya muziki wakidhani kwamba muziki ndiyo mkombozi wao katika maisha, bila kufikiria kwamba hata elimu ingeweza kuwa changamoto ya mafanikio yao katika sanaa.
Wengine hupenda kuiga kufanya kitu fulani kwa kuwa mwenzake anafanya na unakuta hicho anachokiigi hakiko katika damu yake, kwani humsumbua hapo baadaye na kushindwa kukiendeleza.
Wapo pia baadhi ya wakongwe ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakibuni mavazi mbalimbali ambao hawakuweza hata kuwabadilisha Watanzania kwa kuwafumbua macho juu ya ubunifu wa mavazi, wakongwe hao akiwemo Khadija Mwanamboka pamoja na Mustafa Hassanally.
Kwa kweli Watanzania wengi hupenda sana kuvaa mavazi ya kutoka China pamoja na Marekani
kwa kuwa ndizo nguo mabazo ukienda madukani unazikuta kwa wingi.
Wabunifu hawa wa hapa nchini wangeweza kuziweka nguo zao madukani, leo hii tusingekuwa tunavaa nguo zinazotoka China na hata Marekani.
Kijana huyo amekuwa katika fani takribani kwa muda wa miezi minne tu, lakini jina lake linatambulika sana nchi nzima na baadhi ya nguo zake zimekwisha valiwa katika mashindano makubwa hapa nchini ya kumsaka balozi wa Redds.
Katika shindano hilo la kipekee mshiriki kutoka Mkoa wa Tanga Victoria Martin, aliweza kuibuka kidedea katika shindano hilo na kuweza kunyakua taji lililokuwa likishikiliwa na aliyekuwa Miss Tanzania katika nafasi ya pili mwaka jana 2006 Jokate Mwegelo.
Michuano hiyo ilifanyika Jijini Arusha kwani hata vazi alilovaa muongozaji wa shindano hilo siku hiyo Jokate Mwegelo, liliweza kubuniwa na kijana Ally.
Ally anahasili ya Kihindi na pia ni mzaliwa hapa hapa Tanzania, kwani baada ya kuhitimu masomo yake ya Sekondari alitimka nchini kwa madhumuni ya kwenda kuchukua Digrii ya kwanza ya masuala mazima ya ubunifu wa mavazi katika chuo cha Lenght katika jimbo la Pennsylvania na aliweza kuhitimu mwaka jana na kurudi nchini.
Shindano hilo la kumsaka balozi wa Redds siyo hilo tu ndilo alilowahi kushiriki, kwani amewahikushiriki katika maonyesho mbalimbali ya mavazi likiwemo lile la Lady in Red pamoja na Super Model lililofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
Pia mwishoni mwa wiki ya mwezi uliopita kijana huyo mbunifu alizindua mavazi yake yaliyojulikana kwa jina la Prism Break yaliyosheheni katika Hotel ya Movenpic hapa hapa jijini.
Mbunifu huyo alisema ili ufanikiwe unatakiwa ujitume kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwa teyari kwa kuweza kukabiliana na kila kikwazo ambaho kinakuja mbele yako na hakuna mafanikio yanayo kuja bila kusota.
Alisema siri kubwa katika mavazi ni kwa yule mvaaji kuvaa mavazi ambayo yanamfanya awe huru wakati wote wote ule, kwani binadamu anapokuwa huru huonekana amependeza zaidi kutokana na vazi alilolivaa.
Kwani hata kama umevaa nguu ya gharama kiasi gani kama nguo hiyo isipokuweka huru basi tambua kuwa huwezi kuonekana umependeza na matokeo yake unaonenaka kituko kutokana na vazi lako kutokufanya kuwa huru, alisema Ally.
Siri anayoitumia kijana huyu katika kubuni nguo hasa za wanawake ni kusoma maumbo yao na kuweza kutambua anahitaji kitu gani kwa wakati huo na unapofanya biashara ni lazima ujenge ukaribu na mteja.
Pia hutumia matumizi ya malighafi ya asili katika kubuni nguo zake kwani hutumia Khanga na Vitenge katika mavazi yake mengi aliyoyabuni, kwani hulazimika kutumia vitamba kutoka nje pale inapobidi lakini huwa anapenda kutumia lakini huwa hapendi kufanya hivyo.
Mbunifu huyo kwa sasa anajiandaa kufanya maonyesho mbalimbali ndani na nje ya nchi huku akiendelea kubuni nguo nyingine mbalimbali.
Baadhi ya nchi za Afrika ambazo sanaa hii imekubalika ni pamoja na Afrika Kusini pamoja na Nigeria.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala