PISHI LA MBOGA ZA MAJANI
Ninapozungumzia mapishi simaanishi tu pale unapokuwa jikoni ukipika bali mapishi huanza pale unapoandaa, nikimaanisha unapokwenda kununua vifaa unavyovitumia katika mapishi.
Unapokuwa katika hatua hii muhimu ya uandaaji wa mapishi ya mboga za majani yapo mambo muhimu ya kuzingatia katika upishi wako, unapokwenda kununua mboga za majani kwaajili ya mlo hakikisha unanunua mboga nzuri yenye afya na isiyonyauka.
Pia unatakiwa usiweke mboga zako juani wala kwa muda mrefu, kwani kabla ya kuitengeneza/kuichambua na kuikatakata katika vipande vidogovidogo kabla ya kupika hii husaidia mboga isinyauke na kupoteza ubora wake.
Kukata mboga katika vipande vidogo husaidia mboga kuiva kwa urahisi, kwani mboga ya majani haitakiwi kupikwa moto mkali wala kukaa kwenye moto kwa muda mrefu.
Kwa kufanya hivyo husaidia mboga yako kuendelea kuwa na ubora wa kutopoteza vitamini, pia epuka kutumia mafuta mengi.
Pia kuna mapishi ya kuoka mboga za majani, je unaweza kuoka mboga za majani kwa namna gani?
JINSI YA KUOKA.
Unaweza kuoka mboga za majani katika jiko la aina yoyote ile, Oven ya umeme, Gesi, Kuni na hata Mkaa, hii ni kutokana na uwezo wa jiko ulilonalo.
Osha kwanza mboga yako vizuri baada ya kuichambua kisha ikate katika vipande vidogovidogo, iweke katika chomba maalumu na kisafi kwenye Oven. Baada ya hapo kata kitunguu maji, weka na iliki kidogo, vipande vichache vya vitunguu saumu pamoja na mafuta ya kupikia kidogo.
KUOKA KWA KUTUMIA JIKO LA MKAA AU KUNI.
Kwanza kabisa chukua mboga zako ukiwa zikiwa zimeshaandaliwa kama nilivyokupasha hapo juu, chukua sufuria yenye ukubwa kiasi iliyo na maji ndani yake na kisha uchukue mchanganyiko wa mboga za majani pamoja na viungo vyote na kisha uvifunge vizuri katika jani la mgomba.
Baada ya hapo weka suufuria yako jikoni mpaka iendelee kuchemka mpaka utakapoona kuwa imeiva, baada ya hapo wawezakuiepua na kuitoa mboga yako katika mfuko itakuwa imeiva kwani kama hauna jani la mgomb awaweza kuweka hata kwenye mfuko wa nailoni.
Imeandaliwa na Jacqueline

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala