Tafuta DHWTangazaTuandikie
Mapishi ya samaki kwa moshi

MAHITAJI

a/ Samaki mmoja
b/ Chumvi vijiko 2
c/ Mvinyo wa kupikia kijiko 1
d/ Vitunguu maji na vitunguu saumu kila gramu 5
e/ Mchele vijiko 2f/ Pilipili manga gramu 5
g/ Sukari vijiko 2
h/ Asali vijiko 2
i/ Majani ya Cahi kijiko 1

JINSI YA KUMTENGENEZA

1.Kwanza mkate Samaki awe vipande vipande, ondoa kichwa na mkia wake pamoja na uchafu mwingine huku ukiendelea kumkwangua maganda yaliyopo ndani ya mwili wake na baada ya hapo hakikisha unamuosha kwa uangalifu.

2.Baada ya kumuosha vizuri mpake chumvi, mvinyo wa kupikia, vipande vya vitunguu maji na vitunguu saumu.

3.Kisha washa moto na uweke mafuta kwenye sufuria, weka pilipili manga kwenye sufuria uwikaange na kisha ipakue. Mafuta yakiwa na joto la kutosha la nyuzi 70 weka vipande vya samaki kwenye sufuria, vikaange halafu uvitoe.

4.Baada ya hapo weka asali kwenye vipande vya samaki na uviweke kwenye sahani, kisha osha sufuria na uwashe tena na uweke majani ya chai, mchele, pilipili manga na sukari na kisha ukoroge mpaka moshi utokee.

5.Weka sahani kwenye sufuria, endelea kukoroga majani ya chai, mchele, pilipili manga na sukari, halafu zima moto na funika kwa mfuniko na baada ya dakika 5 vipakue.

Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa kazi kwako kula au kutokula.




Imeandaliwa na Jacqueline


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.