MAKANDE
MAHITAJI
a/ Vikombe viwili vya mahindi yaliyokobolewa
b/ Kikombe kimoja cha maharage
c/ Vitunguu maji viwili, kitunguu sahumu
d/ Nyanya mbili
e/ 1/4 Kikombe cha mafuta ya kupikia
f/ Nazi kubwa moja
g/ Pili pili hoho mbili pamoja na Karoti mbili
h/ Binzari kijiko cha chai kimoja, chumvi pamoja na pilipili 1 kali
JINSI YA KUKIPIKA
1. Huku ukiwa umeyaloweka mahindi yako kwani inategemea chakula hichi unakipika lini na kisha yaoshe mahindi yako vizuri na baada ya hapo yainjike jikoni na uyafunuke.
2. Wakati yakiwa jikoni endelea kuyachambua maharage yako na kisha uyaoshe kwa makini, baada ya muda cheki kama mahindi yako yameiva kiasi na kisha uweke maharage ndani ya hayo mahindi na kisha ufunike.
3. Baada ya kama lisaa limoja na zaidi cheki jikoni makande yako yatakuwa yameiva ila yaache yaendelee kuiva zaidi huku ukiwasha jiko lingine bandika sufuria yako jikoni na mafuta kiasi, kisha weka vipande vya vitunguu maji huku vikiendelea kuiva weka pia kitunguu sahumu kilichotwangwa.
4. Vikiiva vyote vizuri weka pia nyaya huku zikiendelea kuiva andaa tui lako la nazi na liwe zito kama kwenye vyombo viwili, nyanya zako zikiiva weka karoti, hoho, binzali pamoja na chumvi kiasi kisha acha kwa muda ili viive na vikiiva viepuwe na umimini katika hakande yako.
5. Kama mafuta hayaja tosha ruksa kuongeza kwani unatakiwa uwache mpaka kuchemke, baada ya hapo weka tui la nazi la pili kwani lile la kwanza liache usiweke kwanza na kisha usiache kukoroga koroga ili tui lisikatike.
6. Ikichemka kwa muda weka tena tui lako la nazi la pili na uendelee kukoroga na ikichemka kwa dakika kadhaa epuwa makande yako ruksa kwa kupakua na kula.
Imeandaliwa na Jacqueline

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala