Tafuta DHWTangazaTuandikie
Yafahamu Mavazi ya Ofisini wakati wa joto

Mavazi huendana na mazingira sehemu husika na nyakati tofauti tofauti, kwani mvaaji anapaswa kujua ni aina gani ya nguo anayopaswa kuvaa na niwakati gani yapaswa kuvaliwa, muda gani au sehemu anayokwenda.

Wengi wao hujikuta wakivaa mavazi mazuri lakini wamekuwa wakionekana kichekesho mbele za watu kwa kuvaa nguo isiyoendana na wakati/sehemu anayokwenda.

Watu wengi wameshindwa kutofautisha nguo za disko, nguo za ofisini hata nguo za usiku na mchana ni zipi, kwani unakuta wengine nguo zinazotakiwa kuvaliwa usiku wao huvaa mchana, kwani nguo za usiku ni zile zenye mng'aro na endapo mvaaji akiutinga wakati wa mchana ataonekana kituko zaidi.

Leo nimeona ni bora nizungumzie mavazi yanayostahili kuvaliwa nyakati za joto, watu wengi wamekuwa wakijiuliza je wanapaswa kuvaa mavazi gani wakati wa joto?

Zipo nguo mbalimbali zinazostahili kuvaliwa hasa katika kipindi cha joto yaani hiyo itakuwa ni kwenda na wakati.

Wanamitindo wengi hushauri sana watu wawe wanavaa nguo nyepesi kwani hii itasaidia upepo kuweza kupita kwa urahisi katika mwili wa mvaaji na kupunguza pia hali ya joto na kumfanya mvaaji ajisikie vizuri.

Usivae nguo ya kuonyesha mikono unapokwenda ofisini kwani nguo hizo huvaliwa nyakati za jioni na pia sehemu maalum, ni vizuri unapovaa nguo za namna hiyo uhakikishe kwamba unakuwa na mtandio mwepesi utakaokusaidia kujitanda ili usionyeshe sehemu ya kwapa.

Usivae nguo za mng'aro sana kwani husababisha joto zaidi katika mwili na pia watu hukushangaa sana pindi upitapo, kwani nguo hizo zivaliwe wakati wa jioni tu na tena kwenye shughuli maalum.

Tunashauriwa pia kutovaa nguo zenye rangi nyeusi wakati wa joto, kwani nguo hizo huakisi jua na hivyo hali ya joto katika mwili huongezeka zaidi.

Kwa upande wa Wanawake wanashauriwa kuvaa zaidi sketi hasa zisizopana sana ili kuweza kuruhusu hali ya joto kupita mwilini kwa urahisi na kupunguza hali ya joto mwilini. Pia kwa upande wa Wananume wanashauriwa kuvaa mashati ya mikono mifupi na mirefu lakini yenye kitambaa cha kotton, kitambaa cha polista kwani vyenye mpira husababisha joto na kumfanya mvaaji kukosa raha.

Usivae Kaptula wakati unapokwenda ofisini kwa kisingizio cha joto, labda tu kama ni sare ya kazi kumbuka pia unapovaa kulingana na wakati mbali na kwenda na wakati kwani itakufanya kuonekana mtanashati.

Pia inashauriwa kuvaa nguo zenye tabaka mbili kwani unaweza kuvaa top na koti jepesi au suti kwa wanaume, hii itasaidia kuendana na mazingira husika ambapo kama joto limezidi sana unaweza kuvua koti na kubaki na top au shati lako kwa upande wa wanaume huku ukiendelea na shughuli zako kama kawaida.

Hakikisha kabati lako lina nguo za aina mbalimbali zinazoenda na nyakati zote, husisababishe kuonekana tofauti.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.