Tafuta DHWTangazaTuandikie
PILAU YA NAFAKA NA NYAMA YA KUSAGA

MAHITAJI

a/ Mchele vikombe 3
b/ Nyama ya kusaga 1 LB
c/ Mchanganyiko wa Nafaka (upendavyo) kikopo 1
(maharagwe, njegere, mbaazi, na kadhalika)
d/ Vitunguu maji kata vipande vipande 3 vya kiasi
e/ Thomu na Tangawizi vijiko 2 vya supu
f/ Mafuta ½ Kikombe
g/ Mchanganyiko wa bizari (Garam Masala) vijiko 2 vya chai
h/ Vipande vya supu (Maggi cubes) 3
i/ Maji (inategemea mchele)
j/ Chumvi Kiasi

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1. Kwanza kabisa unatakiwa kuuchambua mchele, kisha uoshe na uloweke.

2. Baada ya hapo weka mafuta katika sufuria na kaanga vitunguu mpaka viwe brown, halafu uweke Thomu na tangawizi na ukaange kidogo.

3. Kisha weka nyama ya kusaga, chumvi na garam masala, huku ukiendelea kukaanga mpaka nyama iwive na umwaga maji yaliomo katika kopo la nafaka na utie nafaka pekee humo.

4. Weka maji na vipande vya supu (Maggi cubes) huku unavivuruga, koroga kidogo kisha weka mchele na ukoroge kidogo kisha ufunike na upika kwa moto mdogo mpaka ikikaribu kukauka ukikorogoka kidogo na kwa uangalifu (kama unavyopika pilau ya kawaida).

5. Baada ya hapo epua uipike katika moto wa oven 350-400 Deg kwa muda wa dakika 15. na kama sufuria uliyotumia sio ya kupikia katika oven, mimina katika chombo chochote kinachotumika kwa oven kama bakuli la pyrex au treya za foil.

6. Baada ya hapo msosi wako utakuwa teyari kuepuliwa, kupakua pamoja na kuliwa katika sahani.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.