Vaa Pama uende na wakati
Niko nanyi kila wiki kama kawaida yangu na leo nakupa mambo ya Mapama.
Halafu nilivyojehuri nakupa moja kwa moja bila ya kusalimia wala nini! Lakini naona si ustaarabu au vipi! Si kitu , lakini haujambo? Mie kwangu niko poa kwani namshukuru Mungu kwa kunivusha mwaka 2007 na kuweza kuuona tena mwaka 2008, je wewe?
Kuwa nami katika kupeana dondoo za masuala ya mitindo hususani mavazi.
Katika Kona hii leo tutajadili namna bora ya uvaaji wa kofia za aina zote, kwanza nataka tufahamishane aina za kofia kwa majina yaliyozoeleka na wavaaji wake kwani ziko Pama, Kapelo na Baraghashia upo hapo mwakwetu.
Kwa kina nitazungumzia Pama. Pama ni kofia yenye ukingo mpana, na huvaliwa na watu wa jinsia zote na kwa umri wowote, sana sana lilikuwa ni vazi la wapanda farasi huko Ulaya na hata nchini Marekani.
Kutokana na ukuaji wa miji, vazi hilo limesogea hadi kwenye nchi zinazoendelea, wavaaji wengi wa pama katika nchi za Dunia ya Tatu walionazo, pia vazi hilo la pama huwa linafaa hata kwa kazi za shambani hasa kwa wakulima wa mkongwe, miwa, mpunga kule Malaysia, Ufilipino na nchi nyingine za Mashariki Mashariki ya mbali na hata kwa wavuvi pia.
Kwa sasa Pama huvaliwa wakati wa matembezi mbugani au ufukweni. Kofia hizo ni mtindo kwa vijana wawapo kwenye maeneo yao ya kujinadi kama nilivyoeleza hapo awali.
Aidha, Pama ni kofia ya heshima kwa sababu hata Malkia Elizabeth wa Uingereza huvaa pama sanjari na suti yenye hadhi, tena zipo suti zakimataifa ambazo ni lazima zivaliwe na Pama.
Wengi hupendeza zaidi hasa wawapo kwenye starehe katika maeneo ya wazi yenye upepo, wanapovaa pama na miwani ya kuzuia mwanga wa jua (sun glasses) na baadhi yao huvaa pama kukwepa kitu fulani.
Mfano mzuri ni wakati mapaparazi (waandishi, wapiga picha) walipokuwa wakifuatilia kwa karibu kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ditopile Ukiwaona Mzuzuri.
Mtuhumiwa huyo alilazimika kuvaa kofia aina ya pama ili kuzuia mapaparazi wasipate picha yake. Kwahiyo pamoja na kuwa pama ni vazi, pambo pia ni kinga inayopendeza wakati mwingine.
 |

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala