Keki ya Karoti
MAHITAJI
a/ Unga 1 Kikombe cha chai
b/ Baking soda 1 Kijiko cha chai
c/ Iliki ya unga 1/2 Kijiko cha chai
d/ Chumvi 1/4 Kijiko cha chai
e/ Mayai 2
f/ Mafuta 1/4 Kikombe cha chai
g/ Sukari 1/2 Kikombe cha chai
h/ Sukari ya hudhurungi (brown sugar) 1/3 Kikombe cha chai
i/ Mtindi (yogurt) 1/3 Kikombe cha chai
j/ Karoti iliyokaruzwa 1 Kikombe cha chai (kama karoti 2)
JINSI YA KUTENGENEZA
1/Kwanza kabisa washa Oveni moto wa 35°F na baada ya hapo paka chombo chako mafuta ambayo utapikia keki hiyo na kisha unyunyize unga.
2/Baada ya hapo chukua bakuli la saizi na kisha uchanganye pamoja unga, baking soda, iliki kisha uweke na chumvi.
3/Chukua bakuli lingine na upige mayai uchanganye na sukari, mtindi na uweke mafuta mpaka ilainike.
4/Changanya Polepole mchanganyiko wa mayai kwenye unga hadi ilainike na kisha uweke karoti. Na baada ya hapo umimine kwenye chombo ulichotayarisha na uvumbike kama dakika 40-45.
5/Baada ya hapo iache ipoe kwenye sufuria kwa dakika 15 halafu pindua na uiache ipoe kabisa. Na mwisho tengenezasukari laini (icing sugar) 1/2 kikombe na vijiko 2 vya maji na kisha unyunyizie juu na ikisha kauka itakuwa teyari kwa kuliwa.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala