KEKI YA MACHUNGWA
Basi pia siku ya leo tutazungumzia pia upikaji wa keki ya machungwa... kazi kwako kusuka au kunyoa! twende sasa
MAHITAJI
a/ Siagi iliyolainika ½ Kikombe cha chai
b/ Sukari 1 Kikombe cha chai
c/ Mayai 2
d/ Maganda ya chungwa yaliyokwaruzwa 1 Kijiko cha supu
e/ Ariki ya lozi (almond essence) ¼ Kijiko cha chai
f/ Unga wa ngano 2 Vikombe vya chai
g/ Baking powder 2 Vijiko vya chai
h/ Chumvi ½ Kijiko cha chai
i/ Iliki ya unga ½ Kijiko cha chai
j/ Maziwa ½ Kikombe cha chai
k/ Juisi ya machungwa ¼ Kikombe cha chai
l/ Lozi ziliyokaangwa na kupondwa ¾ Kikombe cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1/Kwanza kabisa watakiwa uwashe oveni, na moto uwe kiasi cha 350ºF, na baada ya hapo paka chombo chako siagi ambacho ndicho utakacho chomea (ikiwa unatumia loaf pan ndogo, utahitaji 3)
2/Katika bakuli la mashine, saga sukari na siagi hadi ilainike na kisha weka yai moja moja, halafu ganda la chungwa na ariki ya lozi.
3/Katika bakuli jingine, changanya pamoja unga, baking powder, chumvi pamoja na iliki na uchanganya katika ule mchanganyiko wa siagi, halafu uweke maziwa na juisi ya machungwa, na lozi.
4/Baada ya hapo weka kwenye oveni kwa muda wa dakika 35 na ikiwa teyari epua na iache ipoe na baada ya hapo yafaa kuliwa.
Imeandaliwa na Jacqueline

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala