Tafuta DHWTangazaTuandikie
KUKU WA MAZAGA

MAHITAJI
a/ Kuku 1 mzima
b/ Ndimu 1 au 2, kitunguu saumu, tangawizi na chumvi
c/ Karoti, pilipili hoho, vitunguu maji 2
d/ Bilinganya
e/ Bamia
f/ Maharage ya kijani
g/ Nyanya chungu
h/ Tomato sosi na chili sosi

JINSI YA KUMTENGENEZA

1/ Anza kukatakata kuku mfumo wa vipande vidogo vidogo baada ya hapo uviweke katika sahani na kisha anza kuweka tangawizi iliyotwangwa, kitunguu saumu, ndimu kiasi pamoja na chumvi kiasi.

2/ Baada ya hapo changanya taratibu vipande hivt=yo vya kuku pamoja na viungo hivyo. Baada ya kuchanganya nachukua kikaangio nitakachokitumia kukaanga kuku na kukiweka jikoni, na ninasubiri mpaka kipate mto wa kutosha.

3/ Ndipo naweka mafuta na kuanza kuwaweka kuku hao katika mafuta yaliyopata moto na ninaendelea kuwaacha jikoni waendelee kuiva taratibu kwa kuwageuza mpaka wawe na rangi ya kahawia.

4/ Huku kuku wakiendelea kuiva taratibu naanza kukatakata aina zote za mboga, kwa kuanza naanza kumenya karoti na kuanza kuikata vipande vidogo, nakata pilipili hoho, kitunguu maji saizi ya urefu ili viwe vyembamba.

5/ Huku michanganyiko yote ya mboga ikiwa katika sahani moja naendelea kupasua biringanya kwa urefu, bamia kiasi cha mara mbili, maharage ya kijani nayapasua mara tatu na mwisho nachukua nyanya chungu kukata mara mbili.

6/ Baada ya hapo naipua kuku wangu kwani watakuwa wameiva, na baada ya hapo nachukua sufuria na kuibanika ikoni na ndipo naweka mafuta kiasi na kumimina michanganyiko hiyo ya mboga ndani ya sufuia hiyo na kuzikaanga kwa muda mfupi huku nikiwa nimefunika ili mchanganyiko ulainike.

7/ Baada ya muda nachukua kuku na kuziweka katika mchanganyiko huo wa mboga mbalimbali, huku ukiendelea kuwa jikoni na endelea kukoroga na kuweka chumvi kiasi,tomato sosi pamoja na chili sosi na kuendelea kukoroga taratibu.

8/ Naendelea kufunika kwa muda mfupi kama dakika mbili na ndipo nitaigeiza na kuicheki kama teyari, na baada ya muda naiipuwa na kuiweka pembeni.

9/ Baada ya kuitoa mboga yangu naandaa sufuria ya kusongea ugali, naweka maji ya katika sufuria hiyo ya ugali na kuyainjika jikoni. Huku maji yakiendelea kupata moto wa kutosha nachukua bakuli na kuliweka maji ya baridi na kuanza kukoroga uji mbichi.

10/ Maji yakipata moto wa kutosha namimina uji huo mbichi ndani ya maji hayo yamoto na kuendelea kuukoroga kwa madhumuni ya uji wa kusongea ugali, na nitafunika ili uchemke kwa urahisi.

11/ Naamini uji wangu wa kusonge ugali utakuwa umesha iva na ndipo naanza kusonga ugali, na baada ya muda utakuwa teyari kwa kuepuliwa na kupakuliwa katika sahani teyari kwa kuliwa.



Imeandaliwa na Jacqueline



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.