Tafuta DHWTangazaTuandikie
BIRINGANYA KWA MACARONI

Leo tutazungumzia juu ya upikaji wa Briringanya Kwa Macaroni...!! embu jaribu kupapasa macho yako katika pishi hili la leo...Embu faidi sasa

MAHITAJI

a/ Macaroni PKT 1
b/ Bilinganya 2
c/ Vitunguu maji 2
d/ Nyanya maji 4
e/ Nyanya kopo
f/ Hoho
g/ Karoti
h/ Curry powder
i/ Mafuta
j/ K/Saumu

Namna ya kupika


1/Anza kwanza kukata kitunguu kiasi halafu unawe kitunguu saumu kidogo na kisha anza kukaanga mpaka viwe rangi ya brown, na baada ya hapo weka nyanya, hoho, karoti.

2/Mchanganyiko huu unapokaribia kuiva anza kumenya bilinganya na kukata vipande kiasi unatumbukiza unaacha kwa dk 5, na kisha malizia kuweka nyanya ya kopo, curry powder na chumvi kiasi na baada ya muda mchanganyiko wako unakuwa tayari.

3/Baada ya hapo chemsha macaroni na kisha uchanganye ndani ya sosi yetu ya bilinganya, na baada ya hapo unakuwa tayari kwa kuliwa na pembeni yake hakikisha kuwe na juisi yoyote ile uipendayo ya kuteremshia huo msosi.




Imeandaliwa na Jacqueline


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.