Tafuta DHWTangazaTuandikie
Ni Mrembo pekee anayeendelea kuvuma toka 2007

Tangu shindano la Miss Tanzania 2007 liishe mrembo Victoria Martin amekuwa mrembo pekee anayevuma katika vyombo mbalimbali vya habari kuliko warembo wote walioshiriki shindano hilo mwaka huu, na zaidi ni kwamba amekua akionekana katika kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kuliko hata anavyosikika Miss Tanzania kwani tulitaka kujua nini siri ya mafanikio yake.



“Maisha yangu yamebadilika sana kutokana na kupata tuzo mbalimbali katika mashindano ya urembo ya mwaka huu, kuanzia taji la Miss Tanga, Dollywood Miss Photogenic, Miss Tanzania Kanda ya Kaskazini, na hata kuwa Balozi wa Redds 2007, ” alianza kwa kueleza Victoria mwenyewe.

Alisema anajua umuhimu wake na pia anafahamu kuwa anali jukumu kubwa mbele yake na hata mbele ya jamii iliyomzunguka, na ndio sababu hutumia nafasi aliyonayo na hii isingewezekana kama asingekuwa hapa alipo leo.

Kwani anamshukuru sana Brand Meneja wa Redds, bwana Mpeli Nsekela, pia Meneja wake Asmah Makau jamaa nzima pamoja na marafiki zake waliomzunguka, mawakala wake, wazazi wake na mwisho Mwenyezi Mungu.

Victoria ni msichana pekee aliyebahatika kuwa rekodi nzuri katika mashindano ya Miss Tanzania kutokana na kukubalika na asilimia kubwa ya wadau wa mashindano hayo.

Rekodi ya mrembo huyu ilianza kujiweka tangu alipojikita kwa mara ya kwanza katika ngazi ya vitongoji na kufanikiwa kuvikwa taji la Miss Vyuo, baadaye Miss Tanga, ambako pia alivikwa taji la Miss Photoganic, Miss Tanzania Kanda ya Kaskazini na kisha alitawazwa kuwa Balozi mpya wa Redds baada ya Jokate Mwegelo.

Akielezea tofauti ya maisha yake tangu apate mataji hayo Victoria alisemkuwa “Kabla sijapata mataji hayo nilikuwa sina uwelewa mkubwa katika suala zima la kuihudumia jamii katika masuala mbalimbali.” Anasema sio kwamba alikua hajui jamii inahitaji nini ila alikuwa anashindwa kufahamau njia ambazo zingemuwezehsa kufikisha huduma hizo kwa jamii hiyo.

Anadai kuwa awali alikuwa anajua kuwa jamii inayomzunguka ina matatizo lakini alikua hajui kuwa angeweza kuisaidia kwa namna gani, lakini sasa hivi anajua na tayari amekwisha shiriki katika matukio mbalimbali ya kutoa misaada kwa jamii.

“Nimeshiriki katika matukio mbalimbali ya kusaidia jamii kupitia Ubalozi wangu, na bado nina mpango wa kuendelea kusaidia jamii kwa mfano kamati ya Miss Tanga inanisaidia hivi sasa kukamilisha adhma yangu ya kugawa vyandaru kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Bombo mjini Tanga, ikiwa ni sehemu moja ya kuwashukuru wakazi wa Tanga kwa jinsi walivyoniunga mkono,” alisema mrembo huyo.

Alisema wanampango wa kugawa Vyandarua hivyo kwenye wodi za kina mama ambapo hiyo pia ni moja ya uwajibikaji katika masuala ya kijamii.

Kwa mara ya kwanza Victoria kuonekana akisaidia jamii ilikua katika onyesho la Mitindo la Pink Ribbon, lililokuwa likilenga katika kusaidia kinamama walioathirika na ugonjwa wa saratani ya matiti.

Mrembo huyu alipanda jukwaa katika onyesho hilo kuchangia mfuko wa ugonjwa huo, kwa lengo la kuongeza mashine za kuchukulia vipimo vya ugongwa huo.

Kwani hkuweza kuishia hapo tu kwani aliweza kutembelea vituo mbalimbali vya watoto yatima na kupeleka misaada kidogo.Kupitia Taji la Redds, Victoria alitoa msaada wa pesa taslimu pamoja na vitu mbalimbali kwa ajili ya watoto yatima waishio katika mazingira magumu wa kituo cha St. Benedict kilichopo Mbeya na vituo vya Waterfall
orphanage na.... vya Arusha.

Msaada huo wote wenye zaidi ya thamani ya shilingi milioni moja umekabidhiwa kwa watoto hao yatima na Balozi wa Mitindo wa Redds Victoria Martin akishirikiana na taasisi ya Victoria Expedition, wakati akiwa katika ziara fupi ya Rafda iliyolenga wabunifu wa mitindo ya Kiafrika.

Akikabidhi misaada hiyo Balozi mpya wa Redds Victoria Martin, alisema kuwa ataendelea kutoa misaada ya namna hiyo nchini ili kuwawezesha wananchi mbalimbali wanaohitaji misaada ya namna hiyo ikwa ni moja ya makujikimu yake.

Hivi karibuni Victoria alipanda tena jukwaani katika Tamasha la Maonyesho ya Mavazi lililopewa jina la Tanzania Red Ribbon Gala, lililofanyika kwenye hotel ya Moven Pick ya jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwasaidia watoto yatima na walioathirika na virusi vya ukimwi.

“Kupitia taji la balozi wa Redds nimeweza kuihudumia jamii yangu ipasavyo na nimegundua jamii yangu inahitaji nini, na kama Mungu akinisaidia zaidi hapo baadaye nitaisaidia kwa kiasi kikubwa zaidi,” anasema Victoria.

Mbali na kazi za kijamii Victoria ana ndoto, "Nitakuwa mwenye furaha sana endapo nitafanikiwa kuwa Mwanamitindo wa Kimataifa. Hilo likitimia si tu nitakuwa nimekamilisha ndoto yangu ya muda mrefu, lakini pia itakuwa fursa pekee ya kuitangaza nchi yangu ulimwenguni kote," Maneno haya yalisemwa na Victoria Martin, Mrembo anayeshikilia taji la Miss Tanga 2007, Miss Tanzania Kanda ya Kaskazini 2007 na taji la Balozi wa Redds 2007.

"Nitahakikisha naipepea Bendera ya Tanzania katika Ramani ya mitindo duniani kote, kwa kua uwezo ninao, nia ninayo, na njia ninayo. Na Baada ya kulitumikia taji hili mwakani ninampango wa kupiga hatua nyingine katika mitindo." Anasema Victoria.

Victoria Martin ana umri wa miaka 18, mweupe, mrefu mithili ya Twiga na mwenye haiba na mvuto wa kupendeza, ni mtoto pekee wa kike katika familia ya watoto wanne
wa Mzee Edward Martin Leopold na mama Everlin.

Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Darajani na baadaye alifanikiwa kujiunga na sekondari ya Usagara, ambako alihitimu kidato cha nne, kabla ya kujikita katika mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.

"Matarajio yangu ya baadaye ni kujiendeleza kielimu hususani katika upande wa Mitindo zaidi kwani ataka nije kuwa mwanamitindo wa kimataifa, na inakubidi ufahamu mambo mbalimbali," anasema.

Wito wake kwa wasichana wenzake, anasema; "Napenda kuwashauri wasichana wenzangu hususani wanaojitumbukiza katika fani ya urembo, kutoghiribika na vitu vidogo, na napenda pia kuwaambia kuwa kabla hawajaingia katika masuala ya urembo lazima wao binafsi wajue ni kitu gani kinahitaji katika fani hiyo ili waweze kuwa na muelekeo." Anasema.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.