Tafuta DHWTangazaTuandikie
LEMON BISCUITS

MAHITAJI
a/ Unga wa ngano 4oz
b/ Siagi 2oz
c/ Kiini cha yai 1
d/ Sukari 2oz
e/ Ganda la limiau lililokunwa.

UTENGENEZAJI WENYEWE

1/Paka legeni mafuta, chekecha unga na fikicha siagi hadi mchanganyiko ufanane na chenga za mkate.

2/Ongeza sukari na ganda la limau, kisha uweke ganda la kiini cha yai lililopigwa weka na maji baridi kidogo hadi kiwe laini na kufaa kusukumwa.

3/Baada ya hapo sukuma kinyunga hadi kiwe na unene wa mara 3 kata mviringo ya biscuits, na kisha weka kwenye legeni.

4/Baada ya hapo toboa mashimo ya urembo oka biskuti
kwenye oven zikiiva epua na nyunyiza sukari kama ukipenda.




Imeandaliwa na Jacqueline


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.