Tafuta DHWTangazaTuandikie
Vipande vya nyama ya kuku vyenye ladha ya pilipili na pilipili manga

MAHITAJI:

a/Nyama ya paja la Kuku gramu 500
b/Nusu ya pilipili mboga na nusu ya pilipili hoho
c/Karanga zilizokaangwa gramu50
d/Mchuzi wa pilipili hoho vijiko viwili kiasi
e/vipande vya vitunguu maji
f/vitunguu saumu, tangawizi na pilipili manga na mchuzi vijiko viwili chumvi kijiko kimoja, sukari g/ Mafuta ya ufuta kijiko kimoja, wanga kijiko kimoja, na maji bakuli moja.

JINSI YA UPIKAJI WENYEWE

1/Anza kukata kata nyama ya kuku iwe vipande vipande, bakuli moja, halafu weka mchuzi wa soya, chumvi, sukari, mafuta ya ufuta na wanga huku ukiendelea kukoroga na kisha Piga karanga zilizokaangwa kwa kisu mpaka ziwe vipande vidogo vidogo na ukate pilipili mboga na pilipili hoho ziwe vipande.

2/Baada ya hapo Washa moto na kisha weka mafuta kwenye sufuria, baada ya hapo weka vipande vya vitunguu maji pamoja na pilipili manga na kisha endelea kukoroga vipakue hivyo na tia vipande vya nyama ya kuku, vikaange na kisha uvipakue.

3/Kisha pasha moto tena na uweke mafuta kidogo na baada ya hapo weka vipande vya pilipili mboga na pilipili hoho, vitunguu saumu, tangawizi halafu ukoroge kwa haraka.korogakoroga

4/Ukisha koroga tia mchuzi wa pilipili hoho na umimine maji huku ukiendelea kukoroga mpaka maji yachemke, na kisha weka vipande vya nyama ya kuku na uendelee kukoroga vikiwa teyari vipakue.

5/Mimina vipande vya karanga na vitunguu maji.Kwani Kitoweo hiki sasa kiko tayari kuliwa.




Imetayarishwa na Jacqueline


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.