Mapishi ya vipande vya nyama ya ng'ombe pamoja na mayai
MAHITAJI
a/ Mayai matatu
b/ Vipande vya nyama ya ng'ombe gramu 250
c/ Mchuzi wa soya gramu 5
d/ Wanga gramu 15
e/ chumvi gramu 5
f/ Mafuta ya ufuta kiasi kidogo cha
g/ Pilipili manga
h/ vipande vidogo vya vitunguu maji
UPIKAJI WENYEWE
1/Weka kwanza vipande vya nyama ya ng'ombe ndani ya bakuli moja na kisha mimina mchuzi wa soya, maji kidogo, usisahau kuweka na wanga na umimine mafuta kidogo kisha korogakoroga.
2/Endelea kukoroga mayai halafu weka mafuta ya ufuta, chumvi, pilipili manga, vipande vya vitunguu maji, mafuta kisha korogakoroga.
3/Washa moto tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya nyama ya ng'ombe koroga koroga mpaka viive viweke kwenye mayai yaliyokorogwa.
4/Baada ya hapoWasha moto tena, uqeke vipande vya nyama ya ng'ombe ndani ya sufuria tena, koroga koroga na mimina mafuta kidogo, halafu mimina mafuta ya ufuta, korogakoroga na kisha uvipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
Imeandaliwa na Jacqueline

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala