MISHKAKI YA KUKU
Vipimo:
Kuku kidari (boneless breast) 4 Ratili (LB)
Mafuta ya kukaangia kiasi
Vitunguu 3 Nyanya 3 Pilipili boga 2 Masala Ya Kuroweka Katika Kuku:
Thomu na tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Mtindi 2 vijiko vya supu
Ndimu 3 vijiko vya supu
Chumvi kiasi
Jiyrah (cummin powder/bizari ya pilau) 1 kijiko supu
Dania (coriander powder/gilgilani) 1 kijiko cha chai
Pilipili nyekundu ya unga 1 kijiko cha supu
Mdalasini wa unga 1 kijiko cha chai
**Au tumia ukipenda bizari za mishkaki za tayari kama tanduri masala.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
Kata kuku vipande vikubwa kubwa kiasi .
Changanya kuku na masala ya vitu vyote katika masala ya kurowekea kuku uroweke kwa muda wa masaa.
Katakata vitunguu, nyanya, pilipili boga vipande kiasi.
Tunga vipande vya kuku katika vijiti vya kuchomea kababu (kabaab skewers) huku unatunga baina yake kitunguu, nyanya, pilipili boga.
Tia mafuta kiasi katika kikaango. Mafuta yasiwe mengi hadi yakafunika kuku.
Tumia mafuta kidogo kidogo kila unapoepua kabaab za kwanza ikiwa yamekauka, unaongeza mafuta kidogo kama kiasi ya robo kikombe.
Kaanga kababu za kuku katika moto wa kiasi ukiwa unazigeuza geuza hadi kuku awive.
Epua, weka katika sahani ikiwa tayari kuliwa.
** Waweza kula na chips au ndizi za kuchoma kama si kukaanga....enjoy!!
Imeandaliwa na Alhidaaya.com

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala