Tafuta DHWTangazaTuandikie
valentine Day iyoooo

Februari 14 ya kila mwaka mamilioni ya watu duniani hujumuika kuhadhimisha siku ya Wapendanao 'Valentine Day' kama wanavyoiita wenye lugha yao. Na watu wengi hutumia siku hii kwa kufanyia maasi, uasherati, ngono zembe pamoja na kuonyeshana mavazi ya aibu kwa vijana.



Ni siku iliyoanza miaka 400 huko Uitaliano na baadhi ya watu wakiamini kwamba siku hiyo ilianzia Vatican, kitu ambacho si cha kweli, kwa wengi siku hii hujulikana kama siku ya Mtakatifu Valentine.

Katika Bara la Afrika siku hii imekuwa ikizidi kuongezeka umaarufu wake kila kukicha na siyo kwamba siku hii ina historia ndefu na pana kupita kiasi, bali imejaa historia zenye kupishana kutoka kwa mtu mmoja anayeisimulia hadi mwingine.

Yote tisa historia hizo haziwezi kuibadilisha siku hii au maana halisi ya siku ya Wapendanao na wala siyo ya wanaopendana tu. Licha ya kuwa na tofauti zinazojitokeza kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine na kufikiri kwamba siku hii imetengwa mahususi kwa Wapendanao yaani likizo ya Wapenzi na Mapenzi.

Ni siku ambayo watu walitarajiwa kuwa wanapeana ama kubadilishana zawadi mbalimbali na kuwa karibu sana na wapenzi wao na mambo mengine ya maana hiyo. Naamini kabisa kuwa kama ingewezekana huyo Patron Mtakatifu wa Wapendanao (St. Valentine) akarejea na kuona siku ya kumbukumbu inayosheherekewa, naona angeweza kuzimia kwa mshtuko.

Kwani kipindi nilipoanza kuifahamu siku hii Wapendanao sijawahi kusikia hata siku moja mtu akimtumia mama yake, baba yake, nyanya yake, dada, shangazie, mdogo wake au wakubwa wake, na zaidi iwe ya maana au kadi hata ujumbae mfupi kwa ajili ya kuwatakia kila lakheri katika siku hiyo.

Wengi hukubuhu kwa kufanya uharibifu wa kimapenzi kwa kuitumia siku hii kwa ajili ya kufananisha uovu wao, na imekuwa ikitumiwa na vijana wengi na hata wazee kama siku ya kuwaingiza mkenge mabinti wa watu ambao nao kwa bahati mbaya sana wamekuwa hawana nafasi japo kidogo ya kuhangaisha akili zao katika kufukiri na kutafakari kila waambiwalo.

Ni siku ambayo wapo waliohaidiwa kuzawadiwa/kupewa viatu, magari na zawadi nyingine kemkem mwisho wake wakaishia kuzawadiwa virusi vya Ukimwi. Kwani watu hawa wapo sana katika jamii ya sasa na wala mtu asibishe kuhusu hili.

Pia katika magazeti hasa yale wanayoyaita ya udaku siku chache baada ya siku hiyo ya Wapendanao utakumbana na picha vijana kwa wazee wakiwa wako kama walivyozaliwa, kwani watu mkipendana mpaka muanze kucheza mkiwa uchi/mkalewa na kujisahau mpaka kuanza kufumaniwa na wake za watu au mabinti za watu?

Au kupendana ni lazima muwe na mademu zenu tu ama? Usijidanganye kuhusu hilo hata siku moja kwani unaweza unaweza hata ukapendana na Wazazi wako, ndugu jamaa na hata marafiki zako wa kawaida. Je kwani hatuwezi kupendana na watoto wetu na siku hiyo tukatoka nao pamoja na maam zao tukiwa tumeulamba viwalo vyetu vyekundu na tukaenda mahali kujivinjari nao hadi ile mida mida na kurejea majumbani mwetu tukiwa wapya?

Jamani....Mhhh! nashindwa hata niseme nini kwa kweli wadau wangu kwani hii hali na tunakoelekea naimani itakuja kufikia wakati kuwa siku hii ya Wapendanao itageuka hadi kuwa siku ya kulia kwa kukumbukia yale yaliotutokea katika siyo hiyo.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.