Tafuta DHWTangazaTuandikie
WALI WA DENGU KA SAMAKI WA KUKAANGA



Vipimo

Mchele wa basmati 3 Vikombe
Dengu 2 vikombe Viazi 3 vikubwa Kitunguu 2 kubwa
Nyanya 2
Pilipili mbichi kubwa 3 Pilipilimanga ½ kijiko cha chai Garama Masala (bizari mchanganyiko) 1 kijiko chai
Supu ya vidonge (stock cubes) 2 vidonge
Chumvi kiasi Mafuta ¼ kikombe Zaafarani 1 kijiko cha chai

Samaki wa kukaanga.

-Osha samaki na mtwangie viungo
-vitunguusomu,tangawizi na pili pili manga bila kusahau ndimu na chumvi
-mkaanga

Masala Ya Dengu:

-Zaafarani – iroweke katika maji ya dafu dafu (warm) ya chini ya robo kikombe weka kando.
-Osha mchele, roweka.
-Menya viazi na vitunguu, katakata vitunguu, na nyanya , weka kando.
-Katakata viazi vipande vidogo vidogo kwa umbo la mchemraba (cubes).
-Katika sufuria tia mafuta yakipata moto, tia viazi ukaange kidogo kwa moto mdogo mdogo hadi kukaribia kuwiva, toa weka kando.
-Kaanga vitunguu hadi vigeuka rangi ya hudhurungi isiyokoza (light brown) kisha tia nyanya ukaange kidogo.
-Tia vidonge vya supu (stock cubes) uvivuruge katika mchanganyiko, katakata pilipili mbichi kwa urefu tia, uendelee kukakaanga. Tia bizari, chumvi.
-Zima moto, changanya dengu na viazi katika mchanganyiko huo.

Wali:


-Chemsha mchele kama kawaida ya kupika wali mweupe, kiini kiwe kimewiva nusu yake.
-Chuja maji kisha changanya katika mchanganyiko wa dengu.
-Nyunyizia zaafarani, uchanganye wali na mchanganyiko kidogo tu.
-Funika acha uive katika mtoto mdogo mdogo au tia katika oveni hadi uive kama kawaida ya kupika wali.
-Pakua katiha sahani na tolea na samaki yoyote wa kukaanga.

Kidokezo:

Ukipenda punguza mchanganyiko wa dengu kama vijiko viwili vya supu kwa ajili ya kujaza katika samaki

Imeandaliwa na Alhidaaya.com


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.