KABEJI YA KUKAANZA
Kabeji ¼ kabeji
Karoti 2
Kitunguu 2 viwili
Nyanya 1 Nyanya ya kopo 1 kijiko cha chai
Pilipili mboga 1/2 Chumvi kiasi
Pilipili manga ½ kijiko cha chai
Bizari ya manjano ¼ kijiko Pilipili zilorowekwa katika siki
(hot pepper rings) 2 vijiko supu
(hot pepper rings)2 vijiko vya supu
Mafuta 2 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
-Katakata kabeji, karoti, vitunguu, pilipili mboga, nyanya weka kando.
-Tia mafuta katika karai kaanga vitunguu hadi vilainike na kuanza kugeuka rangi. Usiache vikageuka rangi sana.
-Tia nyanya, nyanya ya kopo, chumvi, pilipili manga, bizari, endelea kukaanga kidogo.
-Tia karoti endelea kukaanga kidogo.
-Tia kabeji na pilipili mboga kaanga kidogo tu.
-Zima moto na changanya na pilipili zilokatwakatwa na kurowekwa katika siki (hot pepper rings) ikiwa tayari kuliwa.
** Unaweza kula na ugali au wali kama kinogeshi cha mchuzi kama zilivyo mboga za majani zingine
Imeandaliwa na Alhidaaya.com

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala