ONEKANA WA KISASA KWA KUVAA VIATU VYA ASILI
Onekana wa kuvutia na Mwanautamaduni kwa kuvaa viatu vilivyotengenezwa kiasili!
Viatu mbali na akuwa muhimu katika kuhifadhi nyayo au miguu lakini pia hutumiwa katika kukamilisha vazi lako ili mvaaji aonekane mtanashati na mrembo pia.
Kwani zipo aina mbalimbali za viatu, vipo viatu vinavyotengenezwa na ngozi, vitambaa, magome ya miti na hata nyuzi a katani. Kwani aina hizo za viatu hutengenezwa kwa mashine na kwa ufundi wa aina yake, lakini zipo aina za viatu ambavyo kwa kutumia malighafi za aina hizo hutengenezwa kiasili kwa mtumiaji hutumia mikono yake kubuni na hata kutengeneza kiatu.
Ninaposema kutengenezwa kwa mikono nadhani unanipata kwani nina maana upo utundu unaofanywa na wanamitindo ambao hutumia mikon0o yao kubuni vitu vya kiasili kama viatu, wabunifu hawa wa kutengeneza viatu vya asili hutumia malighafi tofauti tofauti vikiwapo vitamba, magome ya miti na hata nyuzi za katani pamoja na shanga.
Viatu vya aina hii hupendwa sana na watu wengi hasa watalii wanaofika katika nchi yetu, mbali na kupendwa, aina hii ya viatu pia huonyesha uasili na hata utamaduni wa makabila mbalimbali yaliyopo hapa nchini.
Wabunifu wengi pia hutumia vitu kama shanga, mbegu za matunda au hata simbi katika kunakshi viatu hivyo na kuvifanya vionekane vya kipekee. Kwani viatu vya aina hii hupendeza sana kwani huweza kuvaliwa wakati wowote na waweza kuvalia na vazi la aina yoyote na ukaonekana wa kipekee pia.
Viatu hivi huwa na sifa ya kudumu kwa muda mrefu endapo utavitunza.
 |

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala