Irene Uwoya ageukia filamu
Mmoja wa warembo wa Tanzania ambaye habari zake zimeandikwa kuhusiana mahusiao yake ziliandikwa katika vyombo vya habari, Irene Uwoya, ameamua kugeukia filamu ya Yolanda.
Mtunzi wa filamu hiyo, Lucy Komba alisema juzi jijini Dar es Salaam kwamba, Irene aliyeshika nafasi za juu katika shindano la taifa la urembo mwaka juzi, ameungana na nyota wengine katika filamu hiyo inayosambazwa na Kampuni ya Steps Tanzania.
Lucy alisema kwamba filamu hiyo ina mguso wa aina yake, hasa utatuzi wa matatizo ya wajane wanaobanwa mara baada ya kufiwa na waume zao.
"Imekuwa ni kawaida kwa wajane kuporwa mali na wakwe, mashemeji na mawifi zao ikiwa ni baada ya kifo cha aliyekuwa mumewe kwa ugonjwa wa ukimwi," alisema Lucy.
Alisema kwamba vitendo hivyo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa kina mama ndivyo vilivyosababisha kutunga filamu hiyo ambayo kwa kila atakayeiona atakuwa amepata njia ya kufanya endapo atakumbana na suala hilo.
"Filamu hii imelenga kwenye gonjwa la hatari la ukimwi na uaminifu katika ndoa… yaani nikuelezee kidogo kwamba kuna huyo msanii Frank anajikuta akimtelekeza mkewe baada ya kunasa kwenye penzi la binti mapepe Carolina bila kujali watoto," alisema Lucy na kuongeza kwamba huko ndiko kulikoanza matatizo.
Baadhi ya wasanii walioshiriki mbali ya Frank ambaye jina lake halisi ni Mohammed Mwikongi ni Ummy Wenceslaus 'Dokii', Fadhil Omar 'Mkono', Lucy Komba 'Lorna', Mrisho Zimbwe 'Tito', Dennis Sweya 'Dino', Tecla Irenge 'Nancy', Plicila Christopher, Eva Clemence, Muhogo Mchungu na Goodliver Vedastus.
 |

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala