Tafuta DHWTangazaTuandikie
Adhia awa mlezi wa kituo cha Mkombozi

Miss Tanzania 2007 Richa Adhia amekubali kuwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mkombozi, kilichopo Chang’ombe hapa jijini.



Siku chache zilizopita aliweza kutoa msaada wa vitu mbali mbali kituoni hapo, vikiwemo Mchele, Sukari, Maziwa, Sabuni pamoja na juisi.

Aidha alikubali kuwa mlezi wa kituo hicho, kama alivyoombwa na uongozi wa kituo hicho.

Miss huyo alisema kwamba amefurahishwa na uongozi wa kituo kujitolea kuwalea yatima hao kwa moyo mmoja, na kuwapatia huduma mbali mbali muhumu ikiwemo ile ya elimu ili waweze kukabiliana na maisha yao ya baadae.

Pia katika matembezi ya hayo pia alikuwepo Miss Tanzania liyeshika nafasi ya nne Victoria Martin, naye alijumuika na watoto hao.

Adhia aliahidi kutafuta misaada zaidi kutoka sehemu mbali mbali ili kuhakikisha anashirikiana vyema na walezi hao na kuweza kuboreshea maisha ya watoto kituoni hapo.

Kwa upande wake Mlezi Mkuu wa kituo hicho Michael Maurus alisema kuwa kituo hicho kinakabiliwa na matatizo mengi, likiwemo la kutopatikana kwa vyanzo vya fedha za kuwalipa walimu wanaotoa mafunzo ya elimu ya awali kwa watoto hao.

Shughuli hiyo ni ya kwanza ya kijamii tangu Miss huyo arudi kutoka Sanya, China alipokwenda katika kinyang’anyiro cha kumsaka Mrembo wa dunia Desemba mosi mwaka jana.





 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.