Tafuta DHWTangazaTuandikie
“Salute to Woman hood”

Katika kusherehekea siku kuu ya Wanawake duniani Mbunifu wa mavazi wa muda mrefu Fatmah Amour ameandaa onyesho la mavazi alilolibatiza jina la Festive Collection.

Onyesho hilo lililopangwa kufanyika tarehe 8 Machi, 2008 kwenye ukumbi wa Movienpick limeandaliwa mahsusi kusherehekea siku kuu wa wanawake duniani ambayo ilianza kudhimishwa rasmi miaka 95 iliyopita.

Siku kuu hiyo ambayo ilishasajiliwa na wanawake wafanyakazi na ilianza kuandaliwa kama siku rasmi ya kimataifa na Klara Zetkin wa Ujerumani mwaka 1911 imekua ikiadhimishwa kila tarehe 8 Machi.

Fatma alisema asili ya siku hiyo ni kupigania haki za wanawake na imeendelea kuadhimishwa kuwa ni siku ya wanawake duniani kwa kuwakumbuka wanawake waliotoa mchango mkubwa wa kimaendeleo.

"Wanawake wenzangu waliopambana na mfumo dume bila woga, wanawake waliosimamia misingi ya amani, umoja na upendo, Yapo mengi yanayowakabili wanawake duniani, hayo ndiyo yanayoibuliwa katika siku hii inayoadhimishwa kimataifa ingawa kila nchi inaweza kuwa na kauli mbiu yake kutegemeana na changamoto zilizomo ndani ya nchi husika, mimi nimeona ni adhimishe kwa kuonyesha ubunifu wangu kama changamoto ya kuonyesha wanawake wenzangu kuwa inawezekana," alisema.

Alisema, Onyesho hilo ambalo ni la kwanza kuadhimishwa mwaka huu Ujumbe wake ni “Salute to Womanhood” Akiangalia role ya mwanamke katika jamii yetu kama mama, kama mke na kama mfanyakazi.

Alisema onyesho hilo litapambwa na burudani safi kutoka kwa wanamuziki kama Unique sisterz na wengine


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.