Tafuta DHWTangazaTuandikie
MBAAZI NA MCHICHA



Vipimo:



-Mchicha uliokatwa katwa(chopped)400 gm au vikombe 3
-Mbaazi mbichi au kavu kikombe kimoja - Nyanya kopo ½ kijiko cha chai
-Tui la nazi zito 1 kikombe
-Chumvi kiasi
-Pilipili mbichi nzima 2
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1.*Ikiwa mbaazi sio za tayari, roweka uchemshe hadi ziwive.
2. Osha vizuri mchicha kisha, katakata mdogo mdogo (chopped) au tumia ulio tayari wa barafu (frozen chopped spinach)
3.Katika sufuria, tia mchicha pamoja na mbaazi zilizokwisha iva.
4.Katakata kitunguu, utie humo, tia nyanya kopo, tia chumvi na pilipili mbichi nzima .
5.Tia tui upike katika moto mdogo mdogo hadi zitokote na kuiva mchicha, usiache zikauke sana. Tayari kuliwa na mkate au wali au chapati

Imeandaliwa na Alhidaaya.com



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.