Tafuta DHWTangazaTuandikie
Flaviana aenda kucheki upepo Denmark


Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata,ameenda nchini Denmark kwa ajili ya usaili na mawakala mbalimbali wa wanamitindo .

Flaviana ambaye atakaa nchini Denmark kwa wiki moja ambapo atakutana na mawakala wa hapo na kuangalia kama ataweza fanya nao kazi

“Flaviana ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kimataifa na nina uhakika kuwa mwanamitindo huyu atafika mbali, ndiyo maana Compass Communications tutaendelea kumpa ushirikiano mkubwa” alieleza Maria Sarungi Tsehai, mkurugenzi wa kitaifa wa Miss Universe Tanzania.

Hivi karibuni Flavia alirudi kutoka Budapest, nchini Hungary ambapo alihudhuria sherehe ya kitamaduni inayojulikana kama Budapest Opera Ball.

Mwaliko wa mrembo huyu ilikuja kupitia waandaji wa Miss Hungary.

Mwishoni mwaka mwaka jana alienda kutembea nchini
Ufaransa ambapo pia alifanikiwa kukutana na mawakala wa wanamitindo.

Kila la kheri Flaviana


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.