Tafuta DHWTangazaTuandikie
Richa aanza mwaka kwa kishindo



Baada ya kukaa muda mrefu tangu avishwe taji bila ya kushiriki katika shughuli zozote za kijamii Richa sasa ameanza kazi

wiki hii anatarajia kufanya ziara Moshi mkoani Kilimanjaro kutoa misaada kwa watoto yatima katika vituo mbalimbali zikiwamo fedha taslimu.

Mratibu wa Miss Tanzania Hashim Lundenga alisema Adhia ataambatana na Miss Kilimanjaro 2007, Eva Mbando. Lundenga aliongeza kuwa ziara hiyo ni sehemu ya shughuli za kusaidia jamii ambazo hufanywa na Miss Tanzania kila mwaka.

Ziara ya kwenda kufanya shughuli za kijamii mjini Moshi itakuwa ya pili kwa Adhia tangu alipotwaa taji hilo mwaka jana. Wiki iliyopita alifanya shughuli kama hizo kwenye kituo cha kulelea Yatima cha Mkombozi Dar es Salaam.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.