Tafuta DHWTangazaTuandikie
Filamu zapata tuzo mpya


Baada ya zile tuzo za filamu za Manywele kusua kusua sasa zimeibuka tuzo nyengine mpya ambazo zitatolewa mwezi Mei, ambazo zimeandaliwa wa na One Game Promotions wamesema.


Mwakilishi wa One Game Promotions, Octavian Natalis alisema kuwa zoezi la kupokea kazi za wasanii wa filamu limeanza tangu Machi Mosi na litamalizika Machi 31.


Natalis alisema kuwa kazi za wasanii zinazopokelewa za kuanzia Januari 2007hadi Machi 31 mwaka huu na kuwaomba wasanii wanafuata utaratibu huo.


Alisema kuwa waombaji wa kuingia katika tuzo hizo wanatakiwa kufuata maelekezo yaliyomo kwenye fomu wanazotoa kaa jina la mtayarishaji mkuu wa filamu (Executive Producer), jina la mtayarishaji wa filamu (prodyuza). Mengine ni jina la Mtunzi wa hadithi, jina la mwandishi wa skripti na mambo mengine.


Kwa mujibu wa Natalis, tuzo watakazotoa ni Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa mwaka wa kiume na kike, Muigizaji Chipukizi wa mwaka wa kiume na kike Mwongozaji Sinema bora wa mwaka na Mchekeshaji Bora wa mwaka.


Tuzo nyingine ni Mwandishi Bora wa filamu, Mtunzi Bora wa filamu, filamu bora ya kutisha, Muigizaji Mwandamizi Bora wa kike na kiume Adui Bora wa kwenye filamu, Wimbo Bora wa kwenye filamu wa mwaka na Mhariri Bora wa filamu.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.