Tafuta DHWTangazaTuandikie
Ni Jokate Mwegelo



Haiba, juhudi na uchangamfu na kujiamini kwake kulipelekea kulipelekea wananchi wamvike taji nje ya jukwaa na wadau hawakujuta kwa taji hilo kwani juhudi zake zilionekana na mwaka mzima alifunika na kumfunika aliyevishwa jukwaani pia


Huyo si mwingine namzunguzia mrembo Jokate Mwegole Miss Tanzania namba mbili mwaka 2005, Balozi wa gazeti la Citizen na ni miongoni mwa vijana wa kitanzania wenye vipaji lukuki na mashaallah anavitumia ipasavyo.

Utakumbuka kuwa kabla ya Jokate kutwaa mataji hayo, cheche zake zilianza kuonekana mara tu alipojitosa katika kinyang?anyiro cha kumsaka Miss Kurasini na hatimaye alitwaa taji la Miss Temeke.


Taji la ubalozi wa mitindo wa Redds lilimpa jukumu la kuwa msemaji mkuu wa kinywaji cha Redds ambacho kimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kujenga jukwaa la wanamitindo na wabunifu mbali mbali katika kukuza sanaa hiyo hapa nchini na hivyo kumuongezea uzoefu wa kuongea mbele za watu na kwa kujiamini zaidi.


Jokate ambaye taji lake limerithiwa na balozi mpya wa Redds 2007 Victora Martin, ameweza kujizolea umaarufu na kupendwa na watu wa rika zote, baada ya kuonekana akifanya kazi nyingi za kijamii. Mfano aliwahi kushirikiana na wanajumuiya ya wanafunzi waliosoma katika Shule ya Sekondari Loyola na kutoa msaada katika shule ya watoto wa Shule ya Msingi Mabibo yenye watoto ambao wana mtindio wa ubongo kwa kuwapa vifaa vya darasani na viburudisho.


Mrembo huyu pia alishiriki uchangishaji wa fedha kwa ajili ya hosteli ya wasichana ya Shule ya Sekondari St. Anthony iliyopo Mbagala, ambako mgeni rasmi alikuwa Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.


Tunapomzungumzia Jokate hii Leo historia inajirudia. Ukiachana na historia hiyo, Jokate anasimama kuwa mrembo wa kipekee baada ya kumudu fani mbali mbali kama Uanamitindo, Uigizaji, Utangazaji, U'mc na Matangazo.


Katika uanamitindo Jokate amewahi kufanya onyesha la mavazi la mbunifu mahiri nchini Mustafa Hassanali, na Asia Idarius.

Jokate pia ni Mwigizaji na msimamizi wa shughuli mbalimbali (MC). Kipaji chake katika ulimwengu wa uigizaji filamu kilionekana katika filamu ya Fake Pastors iliyoingia sokoni mwaka jana. Jokate pia anajua kuitumia sauti yake ipasavyo, amewahi kutumika katika kutengeneza matangazo ya redio na aliwahi pia kufanya matangazo ya televisheni.


Unaweza ukadhani kuwa hapa amemaliza lakini aaah wapi!? Jokate ni mtangazaji mahiri wa luninga, aliwahi kupata fursa ya kuonyesha uwezo wake alipopata bingo la kutangaza kipindi cha Bongo Star Search 2006 kwa kipindi cha miezi mitano mfululizo.

Mpaka hapa utakubaliana nasi kuwa huyu bibie ana vipaji vingi na vya aina yake.


Waswahili wasema; Nyota njema huonekana asubuhi. Jokate alizaliwa mwaka 1987 Washington DC nchini Marekani ambako wazazi wake walikuwa wakifanya kazi huko. Waliporejea nchini Jokate alijiunga na shule ya ya msingi Olympio iliyoko jijini Dar es Salaam na baadaye alifaulu kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya St.Anthony.


Shuleni, Jokate zilikuwa zinachaji kiasi kwamba baadaye alifaulu na kuhitimu kidado cha sita katika shule ya Loyola.

Akiwa mwanafunzi wa shule ya msingi Jokate aliwahi kuzawadiwa saa ya ukutani pamoja na kamusi, kutokana na juhudi zake darasani na shuleni kwa ujumla.


Pia aliteuliwa kuwa kiranja, alikuwa akishiriki katika mashindano tofauti tofauti ikiwamo ya lugha ya Kiingereza, ambayo alimudu kuiwakilisha vyema shule yake.


Rafiki zake wa enzi hizo za utoto wake wanakumbuka jinsi Jokate alivyokuwa hodari wa kuandika hadithi fupifupi zinazohusu maisha yake na uzoefu mbalimbali. Jokate pia alipenda kuchora na kupaka rangi katika michoro mbalimbali kwa kuinakshi na rangi tofauti tofauti.


?Nilipokuwa mtoto nilikuwa nacheza michezo yote ikiwemo Rede, Mateka, kamba, kuendesha baiskeli, soka, basketball na mbio za magari, hii ilinisaidia kujenga kujiamini.? anasema akikumbukia enzi hizo.


Akiwa anasoma sekondari Jokate aliwahi kushiriki katika siku ya Kiingereza na Historia shindano lililowakutanisha wanafunzi wa Sekondari ya Pugu na Jitegemee ambapo pia alikuwa akishiriki drama, debate katika lugha ya Kiingereza.


Akiwa mwanafunzi wa kidato cha pili alishika nafasi ya pili katika shindano la Kanda.


Akiwa kidato cha tatu aliweza kuhudhuria semina iliyoandaliwa na shirika la UNICEF lililojadili mada ya HIV/UKIMWI ambapo walipewa elimu juu ya kujikinga na kupambana na ugonjwa wa UKIMWI.


Baadaye aliteuliwa kuwa Katibu wa Vijana wa Umoja wa Mataifa katika mkutano mkuu wa vijana ulioandaliwa na wanafunzi wa shule mbalimbali nchini katika mkutano uliofanyika kwa siku nne huku ukiwahusisha vijana wengi kutoka nje ya nchi ambao pia ni wanafunzi.


Akiwa kidato cha nne alikuwa miongoni mwa wanafunzi wanne walioteuliwa kuhudhuria siku ya Sayansi iliyoadhimishwa katika shule ya wasichana ya Kiislamu Al-Muntazir ambako alishiriki katika michezo ya volleyball, quiz, puzzle solving.


?Mwaka huo huo nilichaguliwa pamoja na wanafunzi wengine saba kuhudhuria mkutano wa njia ya video uliofanyika katika ofisi za Benki ya Dunia mjini Dar es Salaam. Tulikutanishwa na vijana wengine kutoka Uganda na Geneva kujadiliana juu ya teknolojia ya habari ya mawasiliano (CIT?S) na jinsi inavyoweza kutumiwa kirahisi katika kuwaunganisha watu katika masuala yanayowahusu." anaelezea na kuongeza ?Pia kuendesha sherehe za mahafali, kupanga bajeti na wakati huo huo kuhusisha vionjo vingine kama vile mashairi, miondoko stejini, jinsi ya kudansi na kuimba, jinsi ya kuipangilia sauti,? anasema.


Jokate aliwahi pia kushiriki katika siku za vilabu zilizofanyika kila mwaka Loyola High School. Baadaye alichaguliwa kuwa mratibu wa klabu.


Alichaguliwa tena kuwa kiranja wa darasa.

Alishiriki katika shughuli za kijamii, midahalo na kucheza kidogo mpira wa kikapu, mpira wa meza na tenisi pamoja na maonyesho ya mavazi. Aligombea na kuchaguliwa kuwa kiranja mkuu pamoja na kusimamia tamasha la wasichana, ambalo wasichana hujadili masuala yanayowahusu shuleni na katika jamii kwa ujumla. Aliteuliwa kuingia katika shindano la kuandika insha ya Jumuiya ya Madola katika shule ya Shaaban Robert.


Alishika nafasi ya pili na kuzawadiwa cheti na aliyekuwa Waziri wa Elimu na Utamaduni, Joseph Mungai. Ashika nafasi ya pili katika somo la lugha ya Kiingereza kimkoa kidato cha tano.

Alizawadiwa kuwa kiongozi bora wa daraja la juu na mfano wa kuigwa.
picha_4

?Nilijifunza Kifaransa tangu nikiwa sekondari na nilifanya vyema, baada ya hapo niliamua kuendelea kujifunza zaidi lugha hiyo katika kituo cha Alliance Francaise. Pia ningependa kujifunza zaidi Kiswahli, Kiingereza na pia Kihispania." anasema.


Pia alijihusisha na taasisi ya Utamaduni ya Vijana Tanzania (TYC) akifanya kazi kwa kujitolea. Alijihusisha na taasisi ya vijana ya Umoja wa Mataifa (UN) kupitia miradi mbalimbali.

Mpaka hapa najua unatambua kuwa vipaji vyake vina uhusinao mkubwa na makuzi yake, kama nilivyosema; Nyota njema huonekana asubuhi.


Kwa sasa Jokate ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambako anachukua masomo ya Political Science/B.

KIPIMA JOTO<>

Mrembo Jacquline Ntuyabaliwe a.k.a K-lynn alipotua mzigo wa taji la urembo amejikita na katika uanamuzi Je kutokana na historia ya Jokate atajikita kuwa mwanasiasa..... Jinsi ya kushiriki tumpe miaka 3 amalize shule.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.