Waulaya nao kushiriki Miss Tanzania
Washiriki kutoka ulaya wamepewa nafasi ya kushiriki kinyang'anyiro cha kumsaka Miss Tanzania 2008 kwa kuja kushiriki kitongoji cha Miss Elimu ya juu
KAMPUNI ya Lino International Agency, inayoandaa mashindano ya Miss Tanzania, imetangaza mawakala wa ngazi walioteuliwa kuandaa mashindano hayo mwaka huu.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Hashim Lundenga, alisema jana kwamba pamoja na ngazi hizo pia kutakuwa na wawakilishi kutoka nchi za Canada na Uingereza ambako washindi watatu wa kila nchi watashiriki kupitia Kanda ya Elimu ya Juu.
Aidha, wakala wa Mkoa wa Mwanza bado hajapatikana. Mkoa wa Arusha mwaka huu utakuwa na kitongoji kimoja tu cha Njiro kitakachoandaa mashindano hayo kupitia kampuni ya PTA Promotion 2000.
Mawakala walioteuliwa kwa ngazi ya wilaya ni For You Classic Boutique (Geita), Kimkev Entertainment (Bagamoyo), Khadija Sheweji (Kahama) na Vida Salon (Higher Learning Mwanza).
Mkoa wa Dar es Salaam umegawanywa kama mkoa ambako Ilala itasimamiwa na Dar Metropolitan huku vitongoji vilivyoteuliwa vikiwa ni Ukonga (JNC Entertainment), Tabata (Bob Entertainment), Mzizima (Royal Modern Entertainment) na Dar City Centre (Inter Safari Logistic).
Kinondoni itasimamiwa na Boy George Promotions ambako vitongoji vitakavyoandaa ni Ubungo (New Hilux Center), Sinza (Strong Stage Promotion), Dar Indian Ocean (Jacques Collection) na Morocco (Kapitoletaz Entertainment).
Temeke itakuwa chini ya BMP Promotion huku vitongoji vitakavyoandaa ni Chang’ombe (King Promoters) na Kurasini ni ZUM Fashions and Entertainments.
Mikoa na kanda iliyopewa uwakala ni Arusha (Triple A Entertainment), Dodoma (Hedep Enterprises), Iringa (Ebony Entertainment), Kigoma (Samina Arts Production), Kagera (Boom Vibe Explosion), Kilimanjaro (Five Investiment), Lindi (Sky Promotions), Mbeya (Bomba FM).
Wengine ni Morogoro (FG Arts Promotions & Entertainment), Mara (Homeland Entertainment), Mtwara (Big Solution), Manyara (Up to Date Production), Pwani (CMI Entertainment), Ruvuma (Kangsshida Import & Export), Rukwa (Fantastic Entertainment), Shinyanga (Asela Promotions) na Singida Aunt Bora Salon).
 |

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala