Tafuta DHWTangazaTuandikie
TMH kufungua kituo Migomigo

Taasisi ya Tanzania Mitindo House TMH inayoundwa na wabunifu wa mitindo na mavazi maarufu wa hapa Tanzania, inatarajia kufungua kituo cha kusaidia watoto yatima hapo kesho ndani ya Magomeni Mapipa 'migomigo' jijini.



Ufumbuzi huo utaongozwa na mgeni rasmi ndani ambaye ni Mbunge wa Same Mashariki (CCM) Mheshimiwa Anna Kilango wa Malecela.

Naye Mwenyekiti wa TMH Khadija Mwanamboka alisema kituo hicho kinahudumia watoto watano wanaoishi na virusi vya Ukimwi, na kinawasaidia watoto wengine wapatao 25 katika mahitaji yao ya kilasika vikiwemo Vyakula, Mavazi pamoja na huduma ya elimu kwa kila baada ya miezi miwili.

Na kimeweza kuajiri wafanyakazi watano watakao toa huduma kituoni hapo, ni pamoja na Mpishi, Mlinzi, mtu wa usafi, muuguzi na mfanyakazi mmoja wa ustawi wa jamii.

Kwani siku hiyo itakuwa ni siku ya Wanawake duniani, kwani wamewaalika wanawake tu katika sherehe za ufumbuzi ili kwenda sawa na maana halisi ya siku hiyo.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.