Tafuta DHWTangazaTuandikie
Mapishi ya Samaki kwa moshi

Mahitaji:

-Samaki mmoja
-Chumvi vijiko viwili
-Mvinyo wa kupikia kijiko kimoja
-Vitunguu maji na vitunguu saumu kila gramu 5 chai kijiko kimoja
-Mchele vijiko viwili
-Pilipili manga gramu 5
-Sukari vijiko viwili
-Asali vijiko viwili.

JINSI YA KUTENGENEZA

1.Kata samaki awe vipande vipande, ondoa kichwa pamoja na mkia wake, Kisha vikoroge pamoja na chumvi, mvinyo wa kupikia, vipande vya vitunguu maji na vitunguu saumu.

2.Baada ya hapo washa moto na uweke mafuta kwenye sufuria, weka na pilipili manga kwenye sufuria na uikaange halafu ipakue. Mpaka mafuta yawe na joto la nyuzi 70 ndo uweke vipande vya samaki kwenye sufuria na uvikaange na baada ya hapo uvipakue.

3.Osha sufuria na huku uwe umewasha moto na uweke majani ya chai, mchele, pilipili manga na sukari huku ukiendelea kukoroga mpaka moshi utoke na weka sahani kwenye sufuria huku ukiendelea kukoroga chai, mchele, pilipili manga na sukari. halafu zima moto na funika kifuniko. Baada ya dakika 5 vipakue na mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.

,
,


Imeandaliwa na CRI


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.