Kivazi kinachowaheusha kina dada
Kivazi kinachowawehusha kina dada kuliko vazi lengine lolote duniani...unaweza amini kuna watu wameshachagua nguo zao za arusi wanata ziwaje hata kabla hawajapata mchumba?!!
Vazi hilo si lengine bali ni lile Wazungu wanaliita Wedding Dress kiswahili sijui ndo laitwa shela au nashindwa elewa kama shela ni ile yajuu mtaniambia hapa hapa lipi ni lipi
Sasa napenda leo niongelee vazi hilo ambalo ni maalum siku hiyo mara nyingi linakuwa la rangi nyeupe japokuwa siku hzi wanavaa Off White wakidai kuwa hii rangi nyeupe huvaliwa na wanawake mabikira wakati siku hizi mabiharusi wengi huolewa wakiwa wanajawazito kitu kinachowafanya wavae rangi hiyo...ah lakini mie naamini tunavaa rangi iyo ili kuendana na wakati tu na sivinginevyo.
haya magauni hayo siku hzi yanakuwa ya tube dress yake ambayo hayana mikono na yanayoishia kifuani kwani yale yenye mikono haswa mirefu yamepitwa na wakati, japokuwa kuna wengine wanadai hizi tube dress haziruhusiwi makanisani kisa yanaonyesha mabega
mie nawashauri muwe mnazaa na vikoti ay mitandia au lile veli liwe kubwa la kufunika mabega na hadi mgongoni ili mtoke bomba.
Tukio kubwa kama vile kufunga harusi kwa mwanamke ni jambo ambalo hutumia gharama kubwa katika kulifanikisha pamoja na kumgharimu muhusika katika kuhakikisha anapendeza kivazi chenyewe ndo hiki.
 |

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala