Tumepata Mawakala wapya-Lundenga
Ile Kamati ya Miss Tanzania imetangaza mawakala waliochaguliwa kuandaa mashindano ya urembo katika ngazi mbalimbali ambazo hazikuwa na mawakala.
Naye Mratibu wa Miss Tanzania Hashim Lundenga aliitaja kampuni ya Flora Salon and Entertainment, kwamba itaandaa Mwanza huku Manka Salon itaandaa kituo cha Nyamagana.
Lundenga alisema kampuni ya Chiko and Nelly Classic Boutique imepangwa kuaandaa kituo cha Kigamboni.
Maandalizi hayo ni mwanzo wa mbio za kumsaka mrembo wa Tanzania, Miss Tanzania 2008 na mbio hizo zitaanzia kwenye Vituo, Mikoa, Kanda na baadaye Taifa kabla ya kumpata Miss Tanzania atakayeiwakilisha nchi kwenye shindano la kumsaka Mrembo wa Dunia.
Anayeshikilia taji hilo ni Richa Adhia aliyelitwaa mwaka jana baada ya kuwabwaga warembo wengine 26, kwani aliweza kuiwakilisha nchi katika shindano la kumsaka mrembo wa dunia lililofanyika Sanya, China, mwaka jana lakini aliambulia patupu.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala