Miss Utalii 2008 kuondoka na magari kila mmoja
Warembo watakaoshika nafasi tatu za juu katika shindano la kumsaka Miss Utalii 2008 watazawadiwa gari kila mmoja.
Naye Rais wa Miss Utalii Gideon Chipungahelo ilisema tofauti katika magari hayo itakuwa ni bei na si lingine.
Chipungahelo alisema mrembo atayeshika nafasi ya kwanza atapata gari lenye thamani ya Sh milioni 20, wa pili atapata lenye thamani ya Sh milioni 15 na wa tatu atapata lenye thamani ya Sh milioni 10.
Rais huyo alisema lengo la kutoa zawadi hizo ni kuongeza chachu ya mashindano, na zawadi nyingine zitakuwa ni kuwapeleka kozi ya utalii ngazi ya Stashahada washindi wa tano wa mwanzo katika vyuo mbalimbali nchini na gharama yake ni Sh milioni 25.
Alisema sababu ya kuwapeleka warembo hao kozi hiyo ni kuhakikisha mabalozi hao wanatumia elimu, na safari ya kuzunguka nchi nzima kuhamasisha Watanzania masuala mbalimbali.
Naye Aidha alisema kamati yake itahakikisha washiriki katika ngazi ya taifa wanapata vyanzo vya mapato yao ya kila siku kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Sh Milioni 300, na kampuni ya mitindo ya Platinum Model Management ya Uingereza.
Mashindano haya ya Miss Utalii hufanyika kila mwaka ambapo Litha Kavishe wa Kilimanjaro aliibuka Miss Utalii 2007 katika fainali zilizofanyika Dar es Salaam.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala