Tafuta DHWTangazaTuandikie
Bila fedha huwezi kuwalea watoto-Anne

Wanamitindo waliopo ndani ya kamati ya Tanzania Mitindo House 'TMH', wanatakiwa kusaka njia za kupata mikopo pamoja na vyanzo vikubwa vya mapato ili kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.



Changamoto hiyo ilitolewa wishoni mwa wiki na Mbunge wa Same Masharki Anne Kilango Malecela, alipokuwa akizindua kituo cha mitindo na Makazi ya matumaini kwa watoto waishio katika mazingira magumu cha 'Tanzania Mitindo Orphanage Centre' kilichopo Magomeni Mapipa 'migomigo' jijini.

Mama Malecela ambaye ni mwanasiasa machachari alisema kunatakiwa kuandaliwe michakato muhimu ya kuwawezesha kupata fedha, kwani bila kuwa na michakato madhubuti huwezi kupata fedha na bila ya mshiko huwezi kuwalea watoto kama inavyostahili.

Naye Mwenyekiti waTanzania Mitindo House Khadija Mwanamboka hakuwa kimya, alisema licha ya makazi hayo mapya kuzinduliwa kwa ajili ya watoto 30 pia wanahitaji kupata makazi ya kudumu.

Alimalizia kwa kusema endapo watapata makazi ya kuyatawala wenyewe, yatapunguza gharama za uendeshaji ambazo zitawawezesha kuchukua idadi kubwa ya watoto ambao watalelewa kwa kiwango cha juu bila kuhofia kupandishiwa kodi ama kufukuzwa.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.