Jasmine kufyatuliwa mkesha wa Pasaka
Kundi la Sanaa za maigizo ya luninga na filamu linalotesa hapa nchini la Fukuto Art Professional, lilitesa vilivyo katika filamu mbalimbali za kibongo, linatarajia kuzindua tamthilia mpya ya Jasmine.
Tuesday Kihangala ni Mkurugenzi wa kundi hilo na pia ni muandaaji wa uzinduzi huo, alisema uzinduzi huo utafanyika siku ya mkesha wa Pasaka ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee.
Kihanga alisema uzinduzi huo utasindikizwa na kupambwa na burudani kabambe toka kwenye bendi ya Wazee wa Ngwasuma 'FM Academia'.
Alisema baada ya kukamilisha uzinduzi huo hapa nyumbani, pia wataupeleka katika Mikoa ya Mwanza na Arusha.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala