NIDHAMU NDO SILAHA YETU
Ni Isaya Mwakilasa almaarufu kama Wakuvwanga ukipenda muite Mama belee au waziri mkuu mstaafu ndiye kiongozi wa kundi hilo la vichekesho linalotikisa Bongo kwa sasa ambalo lina viumbe vipavyo 6 ambavyo vimebadilisha siku ya alhamis kujulikana kama Ze comedy badala ya alhamis.
Nilibahatika kukutana nao lakini nilianza na huyu Mama Beleee ambaye aliniambia kihistoria alizaliwa miaka ya 70 huko Mpanda Sumbawanga akiwa ni mtoto wa pili kwa mama yake ambaye anadai kafanana nae saaano...'ndo maana akiwa ameuvaa umama Belee anafananiaa .
Elimu ya msingi aliianzia huko huko Sumbawanga na sekondari akaendelea Kantalamba.
Hiki ni kipaji ambacho ninacho mimi kama unavyojua uchekeshaji ni kipaji huwezi igiza kuchekesha wazungu wanaita 'Natural Brain' kitu kipo kwenye damu.
Historia yake katika fani inaanzia mwaka 1999 ambapo alianzia Victoria Arts Group cha jijini Dar es salaam ambacho kilikuwa kinajihusisha zaidi na sanaa za jukwaani, Baada yahapo alijiunga na kikundi cha Kidedea ambacho kilikuwa kinaongozwa na Jenguo na Marehemu Peace ambacho baadae kilikuja kuvunjika na wao wenyewe kujikusanya na kuonyesha tamthilia ya Mboni ya Jicho ambayo ilirushwa Star TV
Baada ya hapoalijiung na kundi la Mizengwe ambalo linatusha vichekesho vyake ITV
ILIPOANZIA ZE cOMEDY
"Ze Comedy ilipoanzia ilikuwa baada ya kualikwa katika show ya live iliyokuwa inaendeshwa na kituo cha televisheni cha EATV maarufu kama Chanel 5 ambapo tuliitwa wachekeshaji wote nchini akiwemo Zembwela,Mtanga, Senga,Joti ,Bambo,Mpoki nk
Wakati show inaendelea tuliulizwa kama swali la uzushi kuwa je tuna uwezo wakuchekesha? tukakubali na tukaona kama chalenge na baada ya show Seki na Seko walituuliza je tunauwezo wa kuchekesha watu mfano tukipewa live show...sie tuliichukulia kama chalenge na tukaanza kujifua na ndipo tulipoibuka na zile Live show ambapo tulikubaliana tuwe tunafanya show na kisha inarushwa kwenye tv na tukaanza na ile ya Slip Way na kisha Star Light
Baada ya vipindi vile kurushwa kuna wengine walishindwa wenyewe na mwendo kasi wetu kutokana na ule moto tuliokuwa tumeanza nao kuna wenzetu ambao waliona wao wako na majina makubwa kushindwa Ze Comedy hivyo ikawa kuna tatizo na wakaamua kujiengua na wengine kutokana na kushindwa kurandana na sisi pia waliondoka hadi mwisho tukajikuta tumebaki mimi, Mpoki na Joti na baadae wakajiunga Masanja, Vengu na Mc Regan na tukatimia watu 6 ambao tupo had leo hii mwaka wapili huu unakuja.
UFANYAJI WAO WAKAZI
Mwanzoni tulikuwa na producer ambaye alijulikana kwa jina la Piccu Tibaz ambaye baadae tuliona hatuendi sawa sababu tulikuwa tunapishana kutokana sisi kuwa comedian yeye hakuwa comedian kitu ambacho tuliona tunapishana ndipo tukaona Seki anatufaa ukizingatia wakati huo tulikuwa tunamtumia kama MC kwenye show zetu.
Na ndipo tulipochekina Seki tukaona anatufaa ukizingatia nae fani hii anaijua fresh hivyo tukawa tunaongea lugha moja na ndio tupo nae hadi leo
USHIRIKIANO ndo silaha yetu kubwa...kwani kila kitu tunafanya pamoja kiasi kwamba inatokea kila anapokuwepo mmoja wa mwana Ze Comedy basi na wengine watakuwepo na kama hatokuwepo ni kutokana na sababu maalum.
....Na hii inapelekea kila mmoja kuwa na nafasi sawa kwenye kundi kwani kila mmoja wetu anaweza kutoa idea na ikasikilizwa na wote tukaipitisha na kisha tunaipeleka kwa MD ambaye nae anaiweka sawa na kutuwashia taa ya kijani....alisema Mama Belee
Alisema wao sio rahisi kuchuja na kuishiwa kama walivyo wachekeshaji wengine kutokana na style yao ya uchekeshaji ulivyo, si wajua sisi tunatumia habari zilizojiri kwa wakati huo na kama unajua habari kila siku zipo ila sisi tunachofanya ni kuzigiza tukiwa na lengo la kuchekesha, kuburudisha , kuelimisha na hata kukosoa
NILITAKA KUJUA VIPINGAMIZI WANAVYOKUTANA NAVYO
...kwani nishasoma kwenye magazeti kuwa wanasambaratika,kuwa watasomewa albadiri na hata kusikia ze comedy watolewa baru kutokana na hii style yao ya kuigiza watu especial viongozi au watu maarufu tofauti.
....Siwezi kuviita ni vipangizi sema ni matokeo ya kazi yetu kwani kusema tumepata matatizo sisi kama sisi hatujawahi kupata kwani uhusika tunaouvaa tukiwa na kwenye Ze Comedy ni tofauti kabisa na sisi kwni tunaweza muigiza mtu lakini tukikutana nae sisi ni watu wengine kabisa tofauti....na kikubwa kinachotupa kiburi ni kuwa tunaigiza vitu ambavyo tunaudhibitisho navyo na watu ambao wamekwishalalamika sie tunawaunganisha kwa MD wetu ambao anamalizana nao...
...Yanayotokea ni mtu kukwambia mbona unamuigiza kiongozi wangu hivyo sasa unachukua jukumu la kumueleweshana nia ya kumuigiza tunashukuru wengi wanatuelewa na kuyafanyika kazi yale tunayoyaigiza ...
WALIYOREKEBISHA
mfano Mbunge wa Kawe Bi Rita alimweleza mmoja wetu kuwa aliona jinsi tulivyogiza yale madimbwi ya maji kule kawe na kuahidi kuyafanyia kazi na kuna mengi tuliyoyakosoa na tuliowakosoa wamejirekebisha kwa ufupi tumefanikiwa.
TOFAUTI YAO NA WENGINE
kwanza ni uwezo wa mungu kutuwezesha kuungana na kuelewana,pili Nidhamu ndio silaha yetu kubwa ndo imetufikisha hapa,tatu tunaichukulia hii kama kazi na hatufanyii hobby ukitukuta tupo kazini tupo busy kama ambavyo mkulima yupo shambani analima na nne style yetu ya kuchukua current issue na kuzifanyia kazi kama unavyojua mambo hayaishi kila siku kuna habari na tano ni kwamba tunamgusa kila mtu kuanzia mtoto, mtu mzima,tajiri, msomi na maskini, viongozi na raia
MAFANIKIO
Nimakubwa kutokana na kila unachopewa yabidi ushukuru lakini madogo ukilinganisha na mafanikio ya wengineo
pili mafanikio ya kupata nafasi Afrika Mashariki ...yaani wana afrika Mashariki kutambua uwepo wetu. na lengine pia tunauhakika wa kula na pakulala yaani tuna maisha mazuri kwa mtanzania yule wa kawaida.
MATARAJIO
Ni mimi kuwa mwaalimu yaani watoto wajifunze kupitia Ze comedy yaani tuwe mfano kwa vizazi na vizazi tuwepo kwenye historia.
Nilitaka kujua watamaintain vipi?
alijibu ni kuepuka tamaa ambayo tuona ndio tatizo la vikundi vingi na tuwe na bidii katika kazi na tusivimbe kichwa kwa kulewa na umaarufu.
Nilitaka kujua kuwa jamaa ana familia??
...Mimi nina mdoli wangu Anaitwa NISA nampenda saana na pia nina mbwa wawili ambao nawaita Tom & Jerry hiyo ndo familia yangu kwa sasa. na ninachoomba mungu sasa anipe mke kwani wasichana wamenitosha.
Nilitaka kumjua anayemkuna katika fani
...aliniambia yeye ni Mr Bean kwani anamuaminia ana uwezo mkubwa mnoo kwani ye akisimama tu anauwezo wakufanya mtu acheke yule ndo comedian. na mwengine anayemheshimu ni Bi Kiroboto wa hapa nyumbani alimtaja kama mchekeshaji wa kike ambaye anaweza.
Alikuwa na Ujumbe
"Usipojiheshimu wewe hatokuheshimu mtu mwengine yeyote"

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala