Tafuta DHWTangazaTuandikie
Kanumba ajitosa kwenye tuzo



Msanii maarufu na mahiri wa filamu Steve Kanumba ameongoza safu ya uchukuaji wafomu za kuwania tuzo wa vinara wafilamu nchini

Akiongea jijini mratibu wa tuzo hizo Khadija Kalili alisema kuwa Kanumba kaanza na anawahimiza na waigizaji wengine wajitokeze kuchukua fomu

Alisema jopo la majaji litakutana baada ya Aprili 18 kuchagua watakaowania tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania 2008.

"Fomu zilizojazwa na nakala ya filamu iliyopo kwenye mfumo wa VCD na DVD zitumwe kwenye ofisi za BASATA zilizopo Ilala Bungoni jijini Dar es Salaam au ofisi ya One Game Promotion," alisema.

Vipengele vitavyoangaliwa na majaji katika filamu hizo kuwa ni Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kike, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kike, Mwongozaji Sinema Bora wa Mwaka,

Vyengine ni Mchekeshaji Bora wa Mwaka, Mwandishi Bora wa Filamu, Mtunzi Bora wa Filamu, Filamu Bora ya kutisha, Muigizaji Mwandamizii Bora wa kike (supporting actor), Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kike, Adui Bora kwenye Filamu, Wimbo Bora wa Mwaka (Sound Track), Mhariri Bora wa Filamu ambao wote watapata tuzo na zawadi. Pia itatolewa tuzo ya heshima kwa wale waliotoa machango wao kukuza sanaa nchini.

Haya kila la kheri!!




 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.