Waridi sambamba na wema
Mnamkumbuka Anne Constantino almaarufu Waridi yule aliyetesa kundi la Mambo Haya wakati huo inavuma katika ITV ameibuka upya.
Baada ya kimya cha muda mrefu Safari hii ameibuka na Mrembo Wema Sepetu ndani ya filamu ya A point of no Return.
Ndani filamu hiyo Waridi anaigiza kama dada wa Wema ambaye anamng'ang'aniza Wema kuolewa na Kanumba,ambapo hataki sikia lalamiko lolote kutoka kwa Wema kumbe...
Kwa ufupi bado yupo fiti katika fani bila shaka huu ni mwanzo na ataendelea kukandamiza katika fani
Cha kufanya isake movie kisha uje tudiscuss kwenye ukumbi wetu wa filamu.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala