Tafuta DHWTangazaTuandikie
Nusu fainali ya visura waTZ



Lile shindano la visura wa Tanzania limefikia patamu ambapo warembo watano wamefanikiwa ingia nusu fainali na wanaenda Johanes Burg,nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya mafunzo.

Visura hao waliingia kambini wakiwa 16 kabla ya wadau hawajawapigia kura ya warembo 6 kutoka ,na jana warembo 5 wengine kuenguliwa na kubaki visura watano ambao wameingia nusu fainali

Warembo hao waliofuzu kuingia nusu fainali ni Edna Makanzo,Emmy Milau,Irene Shirima,Neshino Laizer pamoja na Yvone Ramomi

Wakitangaza warembo hao waratibu wa shindano hilo Irene Kiwia na Nancy Sumari walisema kuwa wakiwa nchini Afrika ya kusini warembo hao watapata nafasi ya kukutana na wanamitindo tofauti akiwemo Happiness Magese 'Millen' na Kaone,kuzuru sehemu za utalii na kuhudhurua fashion show mbalimbali.

Katika safari hiyo visura hao watakaa kwa muda wa siku tano na wataongozana na Balozi wa Redds Victoria Martin

...Baada ya kurejea visura hao April 26 watapanda jukwaani katika ukumbi wa Ubungo Plaza ambapo mmoja kati yao ndio atapatikana na kuwa kisura wa Tanzania na kupata mkataba mnono wa kufanya shughuli za uanamitindo nchini Afrika ya Kusini.


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.