Wajipanga kutoa mrithi wa Richa
Mazoezi ya warembo wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss Sinza 2008 yanatarajiwa kuanza Aprili 28 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mratibu wa shindano hilo kutoka Kampuni ya Strong Stage Promotion, Somoe Ng'itu warembo wote waliochukua fomu wanatakiwa kufika siku hiyo ukumbi wa Vatican City Sinza.
Alisema bado nafasi kwa warembo wengine wenye sifa kujitokeza na kuongeza kuwa mwaka huu Sinza imepanga kutoa mrembo atakayefanya vizuri Miss Kinondoni na hatimaye Miss Tanzania 2008.
Alisema ana imani kubwa kwamba mashindano ya mwaka huu yatakuwa ya aina yake na kusisitiza warembo kujitokeza ambapo zawadi mbalimbali zitakuwepo.
Mshindi wa Miss Sinza 2007 ni Louis Katz, ambapo washindi wanne wa juu wa mashindano hayo watashiriki Miss Kinondoni.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala