Tafuta DHWTangazaTuandikie
Kolelo kuzinduliwa leo



Ni filamu iliyotungwa na mwanadada Irene Sanga mtunzi wa kile kibao cha Salamu zako Mjomba kilichomtoa Mrisho Mpoto

Irene ambaye ni mwanamuziki wa bendi ya Parapanda Arts amesema filamu hiyo imetengenezwa katika mazingira ya kitanzania na wasanii wakongwe katika fani, itazinduliwa leo katika ukumbi wa Dar West Tabata na kusindikizwa na bendi ya FM Academia

...filamu hiyo ambayo imetengenezea katika mlima wa Kolelo zaidi ya kutengenezwa na wakongwe pia inasisimua, inahuzinisha na kufurahisha pia

Waigizaji hao wanaounda filamu hii ni pamoja na Fundi Said maarufu kama Mzee Kipara, Riyama Ally,Tekla Mjata na kuongozwa na Hammie Rajab

Filamu hiyo inazungumzia habari ya ukweli inayohusu mzimu unaoishi kwenye mlima huo tangu karne ya 19 hadi sasa. ambao uliandikwa katika kitabu cha maajabu ya Mlima Kolelo kilichoandikwa na Hammie Rajab


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2008 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.